SHAIRI : BWATUKO - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI : BWATUKO (/showthread.php?tid=1945) |
SHAIRI : BWATUKO - MwlMaeda - 01-03-2022 BWATUKO Mtunzi: Abdul-razaq Rajabu Salimu Shairi: Bwatuko Tarehe: 05/07/2019 BWATUKO 1. Rajabu mwana Salimu, vita sasa nimeanza Naongea mufahamu, maadili kuyatunza Taongea musalimu, kwa wangu huu utunzi Mbwatukaji nabwata, mambo mengi tabwatuka 2. Nabwata kwa mbwatuko, kusudi si kutukana Nabwata kwa sikitiko, kusudi si kugombana Nabwata kwa usikiko, sauti sikike sana Nabwatukia vijana, wakike kwa wakiume 3. Vijana ninyi wa vyuo, ndio nawabwatukia Tena nawashusha vyeo, hasa kwa kuwakamia Mufanyayo huku vyuo, machafu kuyavamia Huu mwanzo wa kubwata, sijui takoma lini 4. Wanikabu na hijabu, leo ninaanza nao Wanamengi masaibu, ni wachafu pia hao Kificho chao nikabu, wazinifu ndio wao Mavazi wayaharibu, uchafu kila uchao 5. Wengine hutekenyana, mwili kusisimshana Mwisho wao kudinyana, vijana kuchezeana Eti ni kula ujana, kutwa kufanyiziana Nabwata mbwatukaji, mchukiao kufeni 6. Wasichana nawachana, metolewa usichana Mulikuja wasichana, munaondoka hamuna Kazi yenu kujamana, chovywachovywa kwa sana Nabwata kwa sikitiko, kusudi ni kuadili 7Mimi ndio mswahili, wa kuenzi uswahili Napenda mambo jamali, hasa yale ya halali Leo meanza na hili, wenzangu tulijadili Nimebwata kwelikweli, haya sasa kosoeni. abuusalahuddiyn@gmail.com Chungwa tamu ni la Tanga |