MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
FASIHI YA KISWAHILI NADHARIYA NA UHAKIKI : MUHADHARA WA NANE - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
FASIHI YA KISWAHILI NADHARIYA NA UHAKIKI : MUHADHARA WA NANE - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Chuo (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=3)
+---- Forum: Shahada (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=20)
+----- Forum: Nukuu (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=22)
+----- Thread: FASIHI YA KISWAHILI NADHARIYA NA UHAKIKI : MUHADHARA WA NANE (/showthread.php?tid=1848)



FASIHI YA KISWAHILI NADHARIYA NA UHAKIKI : MUHADHARA WA NANE - MwlMaeda - 12-27-2021

MUHADHARA WA NANE
   USHAIRI
Ni sanaa ya vina inayopambanuliwa kama nyimbo, mashairi na tenzi. Ushairi una ufasaha wa maneno machache au muhtasari wa mawazo, maono na falsafa za ndani zenye kuvuta moyo kwa namna ya ajabu.
       Sifa za ushairi
–   Wimbo sharti uimbike,ughaniwe na kutongoleka
–   Maneno ya hekima yenye kufunza, kuonya na kuadibu
–   Lugha ya mkato, vina na mizani mf: mfanowe, mefumbata, nk
–   Lugha nzito au lugha ya kunata
Hisiya (lugha inayovuta moyo
Vijenzi vya ushairi wa Kiswahili
Fani na Maudhui
Muwala ni uwiano mzuri kati ya mtiririko wa fikra na umbo la shairi. Mawazo ya shairi yakifuatana kimantiki ubeti hadi ubeti na mstari hadi mstari hufikisha bara bara maudhui yaliyokusudiwa na hapo husemwa kuwa shairi lina muwala.
Muundo ni msuko,mwingiliano na uwiano wa vipengele vyote vinavyojenga shairi au kazi ya sanaa. Vipengele vya kimuundo hudhihirika katika umbo la shairi.
–   Idadi ya beti kwa shairi zima
–   Idadi ya mistari kwa kila ubeti
–   Vipande (ukwapi-utao-mwandamizi)
–   Kituo kila ubeti
–   Mizani
–   Vina
Maudhui ni wazo au mawazo yaliyomsukuma mtunzi wa kazi ya fasihi kutunga kazi ya sanaa. Maudhui huhusisha mtazamo, shabaha na ujumbe.
Umbo hutumika kwa maana ya sanaa ya nje ya shairi au kazi ya sanaa.
Mtindo unakuwa na uteuzi wa maneno; lugha ya Kiswahili huteua maneno maalumu yenye kuleta athari au matokeo yaliyokusudiwa.
–   Takriri- ni mbinu ya kurudiarudia neno au sehemu ya neno kwa lengo la kutia msisitizo.
–   Wizani- ni kiimbo yaani kupanda na kushuka kwa sauti kunakoleta mapigo ya kimuziki.
–   Mchezo wa maneno – ni mbinu ya kutumia maneno ya kiufundi ili kutanua maana ya kile kinachosemwa na kuongeza utamu wa usemaji mfano: wale wali wale wali wao (Mulokozi)
Wale wale ndio wao
Bado wapo palepale
Wao wale wenye vyao
  Na vya kwao vile vile
Wala kale wala leo
Kula huko kura kule
Mwendo huu ndio huo
Bado tupo palepale
–   Lugha ya mkato – shairi huzungumza mambo kwa ufupi kuliko ilivyo katika maongezi ya kawaida. Mfano: shairi la Hila zina maulaya (Amri Abeid)
Nijapotendwa ubaya na wabaya kuwajua
Mwenzi huona haya ubaya kuwatendea
Japo moyo una waya hufanya kuuzuia
Nacheka hali najua hila zinamaulaya
Hila zinamaulaya na wananishambulia
Nyama iliyooza mbaya mbesi hufurahia
–   Taswira – ni mbnu ya kuumba picha ya jambo katika mawazo ya msomaji au msikilizaji kwa kutumia maneno. Mfano: Amina (Shaaban Robert)
Amina umejitenga,kufa umetangulia
Kama ua umefunga,baada ya kuchanua
Nakuombea mwanga,peponi ukubaliwe
Mapenzi tuliyofunga,hapana wa kufungua
          Tamathali za semi
v Sitiari- ni mbinu ya kulinganisha vitu bila kutumia viunganishi linganishi.
Mfano:
–   Elimu ni bahari
–   Misitu ni uhai
–   Kilimo ni uti wa mgongo
v Tashibiha – ni mbinu ya kulinganisha vitu kwa kutumia maneno kama: mfano wa,mithili ya,kama,nk
Mfano:
–   Mrefu kama twiga
–   Mweusi mithili ya kiatu cha jeshi
–   Ananata mfano wa nta
v Tashihisi – ni mbinu ya kuvipa uhai na uwezo wa kutenda kama binadamu vitu au viumbe visivyo na uwezo huo.
Mfano:
–   Misitu ikatabasamu
–   Mawimbi yakapiga makofi
–   Kaburi likamkumbatia
v Tafsida – ni maneno yatumiwayo kwa lengo la kupunguza au kuficha utusi na ukali wa maneno.
Mfano:
–   Ametutoka (kufariki dunia)
–   Kupiga simu ( kwenda haja)
–   Kujifungua (kuzaa)
Ø Mdokezo – ni mbinu ya kumshirikisha msomaji kwa kumuachia akamilishe wazo fulani.
     Mfano:
–   Alipomtazama akamwambia ………… lakini nakupenda.
Ø Ishara – ni matumizi ya maneno yanayoashiria mambo au matukio katika jamii.
Mfano:
–   Mwezi – Baada ya kuona mwezi alirudi nyumbani akiwa na furaha.
Ø Balagha/mubalagha – ni mbinu ya kutia chumvi kwenye habari kwa lengo maalumu.
Mfano:
–   Alikuwa mweusi kama buti la jeshi.
–   Alikuwa mrefu mithili ya twiga
 Mbinu ya kikufu– Ni mbinu ya kukifanya kipande cha mwisho cha ubeti kiwe kipande cha mwanzo cha ubeti au mstari unaofuata.
Mfano:
Kutafuta hali njema, maana ya mapinduzi
Unyonge kuusukuma, uonevu wa majizi
Na kuonewa lazima, tung’owe yote mizizi
Maana ya mapinduzi, Kutafuta hali njema.
 Mbinu ya pindu- Neno pindu katika ushairi lina maana mbili.
(i)         Kufanya neno au sehemu ya neno la kipande au mstari lianze katika kipande cha mstari unaofuata.
Mfano: (Zuko)
Tika kitupu hutika,TIKA upya unafuka
UKA huko ukaleni,LENI mapya kulaFUKA
FUKAra wa mzaMANI, MANI MAPYA hutaKA
TUKATAKA mawazoni,ZONI huna kukuSHIKA
SHIKAmimi sishiKANI,KANIzo zapukutika
(ii)       Mbinu ya kugeuza silabi za neno mwanzo kuwa za mwisho.
Mfano:
Saadan chambilecho, chambilecho humenyeka
Kinyume ni kiambacho,chomba akini hakina
Hila tatu chekecho,chokeche huzipinduka
Kwa wenye chongo kufika,mwe fumba lako jicho
Mbinu ya kidato – Ni mbinu ya kufupisha mshororo mmoja au zaidi kila ubeti kwa lengo maalumu. Malengo maalumu ni pamoja na kupata vina na mizani, kuuliza swali, n.k
Mfano: Nimeamka la S. A. Mohamed
Sidanganywi kwa hotuba na mahubiri matupu
Hata wanakula riba,wanaongoza vikapu
Nimeamka
Nawaambia wahubiri,wanaodanganya watu
Moyo umejaa ari,sizugiki tena katu
Nimeamka
Mbinu ya tungo mchoro – mbinu hii hutumika katika shairi la mchoro ambapo shairi hupangwa katika umbo lenye kufanana na kile kinachozungumziwa hivyo mada ya shairi hilo huonekana machoni licha ya kusikia masikioni.
Mfano: Tafakari tesi
Masikini
Haya ambayo
Mawe yalifinyangwa
na                      maumbile
mawe                          ambayo
yalisongwa                          na
matambara                        maskani
haya                                ambayo
yalimiminishwa                           kwa
saruji                              itokanayo
HISIYA ZA KISHAIRI
Hisiya za kishairi hutokana na msukumo wa ndani ya moyo alionao mshairi wakati anatunga shairi lake.
Aina za hisiya za kishairi
(i)         Hisiya ya furaha
Mfano wa shairi la Cheka kwa furaha
Dhiki ni kama mzaha,asiyecheka nani?
Haya cheka kha kha kha,ndio ada duniani
Basi cheka kwa!kwa!kwa!,usafike moyo wako
 
(ii)       Hisiya za chuki
Mfano shairi la Manzese mpaka Ostabei, 
Unaishi ostabei unapata mchumba/mpenzi Manzese, je atakula nini ilhali hali ya maisha ya manzese yajulikana?
(iii)     Hisiya za kimapinduzi
Mfano shairi la Tohara.
Linahamasisha jamii ya kinamama kuachana na mila za tohara kwa wanawake au wasichana.
(iv)       Hisiya za kichochezi
Mfano: shairi la “Hatumwoni” katika diwani ya Karibu Ndani mwandishi katika shairi lake anasema:
Miungu waliosimama kama vichaka
Waambieni wakae chini warefu
Kaeni chini! Wengi nyuma hatuoni!
Hatutaki vyenu visogo kuona.
Kaeni chini miungu, kaeni chini ndiyo amri!

Mlipewa uongozi ukawapaka rangi
Na madaraka madaraka yakawalevya
Sasa vueni wapisheni wenye nia!

Kokeni mioto mashujaa wa uonevu tuwabanike
Kamwe hapatakuwa na kilio wala matanga
Bali hoihoi za ushindi na madaraka kwa umma

(v)         Hisiya za huzuni
Mfano: Utenzi wa Hayati Sokoine katika diwani ya Mloka.
Ilikuwa redioni
Saa kumi za jioni
Mwenyekiti kwa uchungu
Umma kautangazia