SHAIRI: SINA HARAKA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: SHAIRI: SINA HARAKA (/showthread.php?tid=1793) |
SHAIRI: SINA HARAKA - MwlMaeda - 12-22-2021 SINA HARAKA simiĀ mwenye mamlaka, inipasapo kungoja, Maana sina haraka, najua yajayo yaja, wala sina mashitaka, nikadai jambo moja, Anayejua Rabuka, lipi hasa lenye haja, Na ikiwa hakutaka, aone halina hoja, Simwangushii mashaka, kwa ubaya kumtaja, akisema hili shika, akanipa wake mja, sinipe ninayotaka, kishingo ama kipaja, mie sitalalamika, kishingo sio kipaja! Lolote likinifika, Mola nampa pambaja. Mtunzi Filieda Sanga Mama B Mabibo Dsm 0753738704 |