ETIMOLOJIA YA NENO 'BALAGHAMU' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'BALAGHAMU' (/showthread.php?tid=1753) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'BALAGHAMU' - MwlMaeda - 12-16-2021 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO ' BALAGHAMU' Neno balaghamu katika lugha ya Kiswahili ni nomino yenye maana zifuatazo: 1. Mate mazito yanayokuwa kooni ambayo hutoka mtu anapokohoa; kikohozi kizito chenye utelezi anachotoa mtu anayeumwa aghalabu na kifua Kikuu au homa. 2. Hasira (hutumika katika msemo: 'Toa balaghamu zako; to hasira zako. Katika lugha ya Kiarabu, neno hili balaghamu (soma: balghamun/balghaman/balghamin بلغم ) lina maana zifuatazo: 1. Kohozi: mate yaliyochanganyika na kamasi ambayo hutoka kwenye njia ya upumuaji. Kinachodhihiri ni kuwa neno hili (balghamun بلغم) lilipoingia katika lugha ya Kiswahili na kutoholewa likawa *balaghamu* maana yake katika lugha yake ya asili - Kiarabu - haikubadilika. Shukran sana. Khamis S.M. Mataka. |