NGANO YA "MSAFIRI NA NGAMIA" - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Hadithi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=48) +---- Thread: NGANO YA "MSAFIRI NA NGAMIA" (/showthread.php?tid=1698) |
NGANO YA "MSAFIRI NA NGAMIA" - MwlMaeda - 12-10-2021 Msafiri mmoja aliamua kupumzika kutokana na upepo mkali na vumbi la jangwani. Aliamua kukaa ndani ya hema yake hadi hali hiyo ya hewa ibadilike ndipo aendelee na safari yake. Ngamia wake pale nje alikumbwa na baridi kali hivyo akaamua kumuomba hifadhi ndani ya hema la bwana wake. “Bwana nakuomba uniruhusu nitie kichwa ndani ya hema nijiepushe na athari za upepo na mavumbi yaliyoko hapa nje”. Yule msafiri alikataa na kumweleza kuwa haingewezekana kwani hema lilikuwa dogo. Lakini ngamia alimrairai hadi bwana wake alipokubali. Ngamia alipoona kuwa kichwa chake kiko ndani aliomba aingize shingo yake, akidai kuwa shingo haitachukua nafasi kubwa, naye msafiri alikakubali. Baadaye akakubaliwa kuingiza hata nundu yake na hatimaye akaingiza wote mzima. Msafiri kutanabahi, alikuwa amerushwa nje, huku ngamia akidai kuwa wasingeweza kuenea pamoja kwani hema lilikuwa dogo. Basi msafiri akaumia nje huku baridi inamzizima ingawa hema lilikuwa lake. Hali ya hewa ilipobadilika, msafiri alimwambia ngamia kuwa wangeendelea na safari. Baada ya siku kadhaa hali ya hewa ilibadilika, mvua kubwa ikanyesha naye msafiri akatafuta hifadhi ndani ya hema lake. Licha ya kuwa ngamia alimbembeleza angalau aijiepushe na baridi, msafiri alikuwa ameapa kutorudia kosa lake la awali.
|