MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'SHARUBATI' - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
ETIMOLOJIA YA NENO 'SHARUBATI' - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16)
+--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'SHARUBATI' (/showthread.php?tid=1694)

ETIMOLOJIA YA NENO 'SHARUBATI' - MwlMaeda - 12-08-2021

HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO ' SHARUBATI'

Neno *sharubati* katika lugha ya Kiswahili ni nomino yenye maana zifuatazo:

1. Kinywaji laini ambacho hutengenezwa kwa maji ya matunda au sukari na kisha kutiwa rangi.

2. Kinywaji kinachitengenezwa kwa matunda au maziwa na kutiwa sukari na rangi.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *sharubati* ( **sharubaatun/sharubaatin* *شربات* ) lina maana zifuatazo:

1. Kinywaji kinachotengenezwa kwa maji ya matunda yenye utamu kiasi.

2. Kinywaji chochote mchangayiko.

Kinachodhihiri ni kuwa neno hili ( *sharubati*/ * *شربات*  ) lilipoingia katika lugha ya Kiswahili maana yake katika lugha yake ya asili - Kiarabu haikubadilika.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*