ETIMOLOJIA YA NENO ' MAAKULI' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO ' MAAKULI' (/showthread.php?tid=1693) |
ETIMOLOJIA YA NENO ' MAAKULI' - MwlMaeda - 12-08-2021 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO ' MAAKULI'. Neno *maakuli* katika lugha ya Kiswahili ni nomino yenye maana zifuatazo: 1. Kitu kinachopikwa na kuliwa na kumfanya mtu aishi; chakula cha aina yoyote. 2. Aina mbalimbali za vyakula. Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *maakuli* ( **maakuulun/maakuulan/maakuulin* *ماكول/ماكولا* ) lina maana zifuatazo: 1. Jina la mtendewa wa kitenzi cha Kiarabu cha wakati uliopita *fiilun maadwin* *فعل* *ماض* *akala* *اكل* *(amekula)*;chenye kuliwa, kiliwacho. Wingi wake ni neno *maakulaat* *مأكولات* pia *ma-aakil مآكل* . 2. Chakula chochote kile. Kinachodhihiri ni kuwa neno hili ( *maakuli*/ * *ماكول* ) lilipoingia katika lugha ya Kiswahili maana yake katika lugha yake ya asili - Kiarabu haikubadilika. *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |