MISINGI NA MBINU ZA UUNDAJI WA ISTILAHI - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=9) +--- Thread: MISINGI NA MBINU ZA UUNDAJI WA ISTILAHI (/showthread.php?tid=1648) |
MISINGI NA MBINU ZA UUNDAJI WA ISTILAHI - MwlMaeda - 12-03-2021 [b]Misingi na mbinu za uundaji wa istilahi[/b] Shirika la Kimataifa la Viwango (ISO) ambalo miongoni mwa kazi zake ni kuratibu na kusimamia uendelezaji wa istilahi kimataifa, limeorodhesha kanuni zinazopaswa kufuatwa wakati wa kuunda istilahi katika lugha yoyote. Misingi hii imetokana hasa na mtazamo wa wanaisimu wa Vienna – yaani “Shule ya Istilahi ya Vienna (Austria)” iliyoanzishwa na Eugen Wuster. Kwa muhtasari kanuni hizo zinahusu uundaji wa istilahi lugha moja tu inapohusika na pale lugha mbili zinapohusika. Lugha moja inapohusika kanuni zifuatazo hazina budi zizingatiwe:
(1) Istilahi ziundwe baada ya kupata dhana iliyoelezwa kwa ukamilifu na wazi.
(2) Istilahi ziwe fupi kadiri iwezekanavyo lakini zenye kueleweka. Uundaji wa istilahi kwa vifupisho na akronimia uepukwe hasa kama istilahi kamili si ndefu sana.
(3) Sarufi ya lugha inayohusika lazima itiliwe maanani. Kwa hiyo istilahi ziundwe kwa kufuata mofolojia ya kawaida ya lugha.
(4) Istilahi ziundwe kwa njia ambayo itakuwa rahisi kuunda istilahi nyingine kwa mnyumbuliko.
(5) Uundaji wa istilahi kwa kupanua maana ya neno uepukwe hasa iwapo Nyanja zinazotumia maneno hayo zinakaribiana, ili kuepusha utata. Kwa hiyo mfumko wa sinonimia au homonimia (visawe) hauna budi kuepukwa ili watumiaji wasikanganyikiwe.
Lugha mbili zinapohusika kanuni zifuatazo zizingatiwe:
(1) Uundaji wa
istilahi kwa njia ya kukopa (kutohoa) maneno ya lugha nyingine Uzingatie kuchukua
maneno kama yalivyo katika lugha ya asili na kufanya marekebisho machache tu ili kulingana na sarufi na matamshi ya lugha pokezi. (2) Uundaji wa istilahi kwa kutumia
Kigiriki na Kilatini uendelezwe ili kuzingatia uwakilishi sahihi wa dhana hasa za sayansi na pia kupunguza kishawishi cha kupendelea kutumia baaadhi tu yalugha zinazotumika ulimwenguni hivi sasa Katika uzoevu wa kusanifu istilahi, BAKITA limekuwa likizingatia pia kanuni za nyongeza ili kupata ufanisi zaidi kwa kutilia maanani jamii ya watumiaji wa Kiswahili na utamaduni wake. Kubwa kati ya kanuni hizo za nyongeza ni: (1) istilahi ziepuke utusani – yaani
zisiundwe kwa maneno ambayo tayari yanaeleweka kwamba ni matusi kwa
watumiaji. Kwa mfano katika kutafuta kisawe cha [i]penis, [/i]neno [i]mboo [/i]hushitua
watumiaji wa Kiswahili wengi na badala yake neno [i]dhakari [/i]huvumulika na
kutumika zaidi. Kadhalika kisawe cha neno [i]bone marrow [/i]neno [i]uboho [/i]ingawa
ni sanifu pia lakini huepukwa sana katika matumizi na badala yake neno [i]uloto [/i]limekomaa
sana katika matumizi. Vilevile katika kutafuta kisawe cha neno [i]anus,
[/i]neno [i]mkundu [/i]hushitua watumiaji na neno [i]ngoko [/i]likachukuliwa.
(2) Istilahi ziwe angavu vya kutosha –
yaani istilahi ziweze kudokeza dhana liliyokusudiwa kwa kina na usahihi
kadiri iwezekanavyo. Wakati wa kutafuta kisawe cha neno [i]flip chart [/i]kwa
Kiswahili kumekuwa na pendekezo la neno [i]bango kitita. [/i]Katika
kulichambua neno hilo imedhihirika ya kwamba ingawa neno [i]bango [/i]kwa kiasi fulani
linawakilisha ukubwa wa [i]chart [/i]lakini dhana ya [i]flip[/i] haijidhihirishi. Hivyo halina uangavu wa
kutosha. Pendekezo linaloelekea kupendelewa ni [i]chati pindu [/i]kwa kuwa neno hilo linawakilisha dhana ya [i]chart[/i] na pia utumiksji wake wa [i]kupinduliwa [/i]wakati
chati hiyo inapotumiwa. (3) Istilahi ziwe na ulinganifu wa
mtiririko ulio katika dhana za kikoa kimoja. Katika hili ni muhimu kwa wasanifishaji
kukumbuka kwamba istilahi hazikai pekepeke. Hazifiki mbali iwapo zitasimama
pasipo kuhusisha maneno mengine yaliyo katika uga huo. Istilahi ni kama
matundu ya wavu ambayo kila moja sharti ligusane na lenzake ili hatimaye
mfumo mzima wa wavu uweze kutengenezwa. Kwa hiyo istilahi moja iwe
chanzo cha kupata istilahi zingine kutokana na kuinyumbulisha na kuunda
istilahi zinazohusiana katika uwanja ule. Kwa mfano: [i]Sumaku (magnet),
Usumaku (magnetism), Sumakisha[/i] [i](magnetise), Jisumakisha (auto
magnetise), Usumakishaji (magnetization), nk.[/i] (4) Istilahi zilizozoeleka au kukomaa
kutokana na kutumika kwa muda mrefu zisibadilishwe. Kanuni hii ni muhimu
sana katika ukubalifu wa istilahi zinazoundwa. Ni muhimu kabla ya kuunda
istilahi mpya kuchunguza iwapo hakuna istilahi inayotumika tayari
ambayo inawakilisha kw usahihi dhana inayokusudiwa. Uzoevu wa BAKITA
umeonyesha kuwa ni vigumu kwa istilahi mpya kukubaliwa na kushamiri pale ambapo
tayari kulikuwa na istiahi zilizokuwa zikitumika, hasa zile za muda
mrefu. Kwa mfano neno [i]Ovataimu[/i] [i](overtime) [/i]lililokuwa
limezoeleka kwa muda mrefu limeendelea kutumika badala ya neno [i]ajari[/i]. Vivyo hivyo
badala ya neno [i]Mwia. [/i]Maneno yoteneno [i]Mdai [/i](creditor) limeendelea kutumika mawili ni ya siku nyingi lakini neno [i]mdai [/i]limezagaa zaidi katika matumizi kuliko neno [font="times new roman", serif][i]mwia. [/i][/font] |