VITENZI VYA KISWAHILI SANIFU - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=9) +--- Thread: VITENZI VYA KISWAHILI SANIFU (/showthread.php?tid=164) |
VITENZI VYA KISWAHILI SANIFU - MwlMaeda - 06-21-2021 Aina hii ya neno huweza kufafanuliwa kwa kutumia vigezo mbalimbali vya kiisimu ambavyo ni; kisemantiki, kimofolojia na kisintaksia. Hata hivyo maana inayotokana na semantiki ndiyo huegemewa zaidi. Tazama hapo chini namna ya kufasili kitenzi kwa kutumia vigezo mbalimbali. Kisemantiki, kitenzi ni aina ya neno inayotaja tendo au hali ya kuwa. Kwa mfano;
Kisintaksia, kitenzi ni aina ya neno ambayo hupokea nomino au kiwakilishi mwanzoni na hupokea nomino au kiwakilishi au kielezi mwishoni. Kwa mfano, neno lililoandikwa kwa herufi mlalo ni kitenzi; 1. Musa analima. 2. Justina anatembea polepole. 3. Wewe ni mwanafunzi bora. 4. Tanzania imepata rais. AINA ZA VITENZI Kisemantiki, kuna aina tatu za vitenzi. Aina hizo ni; kitenzi kikuu, kitenzi kisaidizi na kitenzi kishirikishi. Kitenzi Kikuu Ni aina ya kitenzi ambacho humiliki uhusiano baina ya vipashio arifu katika tungo au sentensi. Hii ni sehemu muhimu ya sentensi kwani bila kitenzi kikuu sentensi haikamiliki. Pamoja na kuwa sentensi zote si lazima zikamilishwe na kitenzi kikuu, lakini kitenzi hiki ndicho kinachobeba taarifa nyingi zaidi. Tazama mifano ifuatayo, neno lilioandikwa kwa herufi mlazo ni kitenzi kikuu. 1. Mama anafua nguo za watoto.
Ni kitenzi ambacho uamilifu wake ni kukisaidia kitenzi kikuu kukamilisha uarifu wake. Hii ina maana kuwa vitenzi visaidizi haviwezi kusimama peke yake bila kuwa na kitenzi kikuu. Vitenzi hivi hutoa taarifa ya ziada kuhusu tendo. Vivyo hivyo, vitenzi hivi vikiondolewa katika sentensi haviathiri maana ya sentensi. Tazama mifano ifuatayo, neno lililoandikwa kwa herufi mlazo ni kitenzi kisaidizi.
Hiki ni kitenzi ambacho huonesha zaidi hali ya kuwa. Pamoja na hilo, kitenzi hiki huonesha uhusiano uliopo baina ya nomino au kiwakilishi kinachotajwa na tabia au hali inayozungumzwa. Vitenzi vishirikishi vyote lazima viwe na pande mbili. Upande wa nomino au kiwakilishi na upande wa sifa au hali. Tofauti na vitenzi vikuu, vitenzi hivi haviwezi kusimama pekee na kutoa maana. Tazama mifano ifuatayo, neno lililoandikwa kwa herufi mlazo ni kitenzi kishirikishi.
RE: VITENZI VYA KISWAHILI SANIFU - MwlNkonosha - 06-21-2021 Bwana Maeda,umeweza kuonesha vizuri tabia za vitenzi.Kuna jambo ambalo huwa linanichanganya kuhusu hizi dhana mbili; Tabia na kazi za vitenzi.Kwa nini baadhi ya Tabia hizo ulizozitaja zinaonekana kuingiliana na kazi za vitenzi,mfano kuonesha nafsi?.Asante. Au kazi hasa ya vitenzi vya kiswahili sanifu ni ipi? |