NYAKATI ZA KISWAHILI - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=9) +--- Thread: NYAKATI ZA KISWAHILI (/showthread.php?tid=1611) |
NYAKATI ZA KISWAHILI - MwlMaeda - 11-28-2021 Nyakati za Kiswahili
Nyakati katika lugha hutuonesha kitendo chafanyika lini.
Mifano ya Nyakati
Wakati Uliopita – LI
Wakati huu hurejelea kitendo kilichofanyika muda mrefu uliopita. Vitenzi katika wakati uliopita hutumia kiambishi “LI”
kwa mfano : a-li-sema, ni-li-fika, wa-li-timuliwa
Wakati Timilifu – Uliopita Muda Mfupi – ME
Wakati timilifu huonyesha kitendo ambacho kimekamilika sasa hivi au muda usio mrefu. Hutumia kiambishi ME katika vitenzi.
kwa mfano: nimeshiba, limeanguka, kimeharibika
Wakati Uliopo – NA
Wakati uliopo huonyesha kitendo kinachoendela kufanyika sasa hivi. Hutumia kiambishi “NA” katika vitenzi.
kwa mfano: a-na-soma, tu-na-kueleza, zi-na-angamia
Wakati Ujao – TA
Huchukua kiambishi “TA” na hurejelea kitendo ambacho bado hakijafanyika lakini kinatarajiwa kufanyika..
kwa mfano: atakupa, kitajulikana, utapokelewa
Wakati wa Mazoea – HU
Hutumia kiambishi “HU” na hurejelea kitendo ambacho hufanyika mara kwa mara au kila siku n.k.
kwa mfano: hutembea, husoma, huzilinda
Wakati Usiodhihirika – A
Hutumia kiambishi cha ngeli au nafsi pamoja na kiungo “A” kurejelea kitendo kinachoendelea kutendeka katika wakati usiodhihirika.
kwa mfano: achukua, zapepea, twaangamia
Wakati Timilifu Usiodhihirika – KA
Hutumia kiungo “KA” kurejelea kitendo ambacho kinakamilika katika wakati usiojulika. Pia hutumika kurejelea kitendo kifanyika baada ya kingine. Hutumiwa katika masimulizi.
kwa mfano: ikawalemea, tukazichukua, likampendeza
|