MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

UBORA NA UDHAIFU WA NGELI ZA KISINTAKSIA/KISASA - Printable Version
|

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=9)
+--- Thread: UBORA NA UDHAIFU WA NGELI ZA KISINTAKSIA/KISASA (/showthread.php?tid=1579)
|
UBORA NA UDHAIFU WA NGELI ZA KISINTAKSIA/KISASA - MwlMaeda - 11-27-2021
UBORA WA MTAZAMO WA KISASA
Kigezo cha kisintaksia kinachotumiwa katika mtazamo wa kisasa kugawa ngeli kwa kuzingatia upatanisho wa kisarufi kina ubora wake kama ifuatavyo: - Kimepunguza makundi mengi ya ngeli za nomino
- Ni rahisi kuzikariri kwani ni chache.
- Kila nomino huweza kuingia katika ngeli yake kwa kuzingatia upatanisho wa kisarufi.
- Nomino hupangwa katika ngeli zake kulingana na sifa na hadhi yake.
- Husaidia kubaini umoja na wingi wa nomino zisizo na maumbo dhahiri ya idadi.
- Kigezo hiki kimepunguza kujirudiarudia kwa ngeli.
- Husaidia kubainisha uhusiano wa nomino na maneno mengine katika tungo.
- Husaidia kuonesha urejeshi wa vitenzi na nomino zake.
UDHAIFU WA MTAZAMO WA KISASA - Bado kuna ngeli za nomino zinazojirudia mf. Ngeli ya 2,6 na 7 umoja zinatumia u.
- Ngeli ya kwanza umoja ina viambishi viwili (Yu/A)
- Bado kuna nomino zenye kuleta mgogoro katika ngeli mf. Makala, Jambazi, marashi.
- Pamoja na umoja na wingi kutawala, kigezo cha sifa ya nomino hujitokeza ili kuepuka kuchanganya majina yenye sifa na hadhi tofauti mf. Kinyonga hukubali zaidi ngeli ya (KI-VI) lakini huwekwa katika ngeli ya kwanza kwa sifa ya kiumbe hai.
- Kigezo hiki hakijaweza kuonesha mofolojia ya nomino.
|