DHANA NA DHIMA YA -O- REJESHI - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=9) +--- Thread: DHANA NA DHIMA YA -O- REJESHI (/showthread.php?tid=1572) |
DHANA NA DHIMA YA -O- REJESHI - MwlMaeda - 11-27-2021 Fasili: -0-rejeshi ni kiambishi cha mtenda au mtendwa ambacho hujitokeza katika kitenzi au amba- ili kuonesha dhana ya urejeshi. Urejeshi huo hufuata mfumo wa upatanishi wa kisarufi yaani mfumo wa ngeli. Ngeli ni utaratibu wa kupanga majina ya Kiwahili katika makundi yanayofanana. Kiambishi hiki hujiegemeza kwenye kiambishi ngeli cha nomino iliyotajwa. Viambishi vya –o- rejeshi ni kama vile -ye-, -o-, -cho, -mo-, -vyo- Kwa mfano:
Katika -o- rejeshi vitenzi hubeba viambishi ngeli vyenye kiangami -o- isipokuwa kama nomino iliyotajwa ni ngeli ya kwanza umoja. Urejeshi wa ngeli hiyo hutumia -e- badala ya -o-. Hivyo, -ye- ni -o- rejeshi kwa kwa inaangukia kwenye ngeli ya kwanza (YU/A-WA) hata kama haina -O- Swali: Taja mazingira matatu ya kisarufi ya utokeaji wa -o- rejeshi katika tungo. Kiambishi cha -o- rejeshi hujitokeza katika mazingira yafuatayo: Mosi hujitokeza kabla ya mzizi wa kitenzi. Kwa mfano:
|