Utata wa Sentensi - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=9) +--- Thread: Utata wa Sentensi (/showthread.php?tid=1564) |
Utata wa Sentensi - MwlMaeda - 11-27-2021 Utata wa Sentensi
Sentensi zifuatazo, bila shaka tutakubaliana, ni rahisi na za kawaida sana katika Kiswahili:
Quote: Ikiwa sentensi hizi zitasikika bila kuwekewa mazingira yanayopasa, mjua Kiswahili yeyote atatambua kuwa kila mojawapo ya sentensi hizi inaweza kuelewekwa kwa namna zaidi ya moja.
Katika sentensi ya (1) tunaweza kuwa na wahusika wawili au watatu:
Quote: Sentensi ya (2) vile vile, tunaweza kuielewa kama (a) au (b):
Quote: Halikadhalika, sentensi (3) inaweza kueleweka kama (a) au (b):
Quote: Utata wa sentensi za hapo juu hautokani na tofauti za kimuundo katika sentensi hizo, kwani miundo yao inafanana kama vielelezo vya hapa chini vinavyoonyesha:
Taswira Taswira Taswira Sentensi zote za hapo juu zimegawanywa katika kuma na prediketa. Hata vipashio vinavyo jenga kiima na prediketa pia vinafanana. Hivyo kiima kimejengwa na nomino, au nomino’na kivumishi; prediketa imejengwa na kiarifu na kishamirishi; kiarifu kimejengwa na kitenzi, na kishamirishi kimejengwa na nomino (au nomino na kivumishi). Mahusiano ya wahusika katika sentensi hizi, ambayo ni chanzo cha utata, hayadhihtriki katika muundo wa sentensi hizi kama zinavyooonekana. Wazungumzaji wanatafsiri au wanazielewa sentensi tata kama hizo hapo juu kwa sababu wanao ujuzi wa mahusiano ya ndani ya sentensi hizi.
Kwa upande mwingine, tunaona kuwa sentensi inayofuata, ingawa ina muundo sawa na sentensi za hapo juu, haina utata kama wa sentensi za hapo juu:
Quote: Katika mchoro, sentensi hiyo itaonekana kama ifuatavyo:
Taswira Kukosa utata kwa sentensi hii kunatokana na maana na matumizi ya kitenzi “iba”. Kutokana najinsi tunavyoelewa neno hilo katika matumizi ya kawaida, mtu hatazamiwi kujiibia mwenyewe, na hivyo katika (4) kitabu hakiwezi kuwa cha Ali. Sentensi hii itaeleweka kwa njia moja tu kama (4a):
Quote: Hapa tunaona kuwa hata kitenzi kinachotumika kinaweza kuifanya sentensi ieleweke kwa njia tofauti. Katika sentensi (5) bado tunaweza kuona utata, ingawa muundo wake ni kama wa (4):
Quote: Utata wa sentensi hii utaonekana ikiwa tutafikiria mazingira ya aina mbili:
Quote: Ili kutambua kuwa ujuzi wa lugha alio nao mwanadamu ni changamano, yaani unajumlisha vipengele vingi, angalia sentensi zifuatazo na kuzilinganisha na baadhi ya zile ambazo tumeziona hapo juu:-
Quote: Ikisemwa hivyo, (6) itaeleweka tu kama (2a), na haiwezi kueleweka kama (2b).
Na kama tutalinganisha sentensi ifuatayo na ya (3) tutaweza kuona pia kuwa inaweza kueleweka kwa njia moja tu:
Quote: Hapa sentensi hii inaweza kuchukua tu maana ya (3a) na siyo Ue ya (3b).
|