VYOMBO ( ASASI ) MBALI MBALI VYA KUKUZA NA KUENEZA KISWAHILI NCHINI - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Taasisi za kukuza lugha (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=18) +--- Thread: VYOMBO ( ASASI ) MBALI MBALI VYA KUKUZA NA KUENEZA KISWAHILI NCHINI (/showthread.php?tid=1151) |
VYOMBO ( ASASI ) MBALI MBALI VYA KUKUZA NA KUENEZA KISWAHILI NCHINI - MwlMaeda - 09-06-2021 Baada ya uhuru, serikali imechukua hatua mbali mbali ili kukuza na kueneza Kiswahili . hatua moja wapo ni ile ya kuunda asasi za ukuzaji Kiswahili. Asasi hizo ni:
Hiki ni chama cha Usanifu wa Kiswahili na Mashairi . chama hiki kilianzishwa mwaka 1965 na mshairi Mathias Mnyapala kwa lengo la kukuza ushairi wa Kiswahili kwa ujumla.
Ukuta ilikuwa na malengo yafuatayo:
a). Kukuza lugha ya Kiswahili na ushairi kwa ujumla kwa njia ya kujishughulisha na kazi tafauti zinazohusiana na maendeleo ya Kiswahili na ushairi kama vile uhariri wa miswada ya Kiswahili, utunzi wa mashairi na uandishi wa vitabu na kutafsiri maandishi mbali mbali katika Kiswahili.
b). Kukuza utunzi wa ngonjera na kuhamasisha utunzi wa vitabu katika misingi yenye kuzingatia utamaduni wa Mtanzania.
Mafanikio ya UKUTA.
c). Imeweza kuundaa na kuendesha semina na makongamano ya Kiswahili na kutunga kazi za fasihi kwa kushirikiana na vyombo vingine.
d). UKUTA imeweza kuandika vitabu mbali mbali vya ushairi hususan vya ushairi, kama vile Ngonjera za ukuta ( cha kwanza na cha pili – 1968 ), Mashairi ya Azimio la Arusha – 1974 na Mashairi ya miaka kumi ya Azimio la Arusha – 1977.
e). Imeweza kutafsiri kwa Kiswahili maandishi mbali mbali . mfano , iliwza kutafisiri majina ya baadhi ya mitaa ya jiji la Dar – es – Salaam kama vile mtaa wa uhuru badala Independence Avenue na mtaa wa Sokoine badala ya Sokoine Drive.
Taasisi hii kihistoria ilianzishwa mwaka 1930 ikiwa kamati ya lugha ya lugha ya Afrika Mashariki na uatwala wa Waingereza , na mnamo mwaka mwaka 1964, ilipandishwa hadhi na kuhamishiwa katika chuo kikuu cha Dar –es – Salaam baada ya kuimarishwa kwa sheria ya Bunge ya mwaka 1964. Na mwaka 1970 kilipoanzishwa chuo kikuu cha Dar –es Salaam taasisi ilikuwa moja wapo wa asasi za utafiti wa chuo, ambapo mpaka leo asasi hii imekuwa ikifanya kazi chini ya Chuo Kikuu,
Mnamo mwaka 2009, taasisi hii ilibadili jina baada ya kuungana na Idara ya Kiswahili ya chuo na kujulikana kwa jina la Taasisi ya Taaluma za Kiswahili. ( TATAKI ).
Malengo ya TUKI ( TATAKI ).
i). Kuichunguza na kuiendeleza lugha ya Kiswahili katika fani zake zote ikizingatia mipango ya muda mrefu katika Jamhuri ya Muungao wa Tanzania, Afrika na mashariki na Katika chuo kikuu cha Dar es Salaam.
3.BAKITA ( Baraza la Kiswahili Tanzania).
Baraza hili liliundwa mwaka 1967 kaw sheria ya Bunge Na. 27. Ya mwaka huo.
Malengo makuu ya uundwaji wa baraza hili ni kutaka kuwepo kwa chombo nchini cha kusimamia shughuli za ukuzaji Kiswahili.
KAZI ZA BAKITA.
i). Kuhimiza matumizi ya Kiswahili fasaha, kuandika vitabu vya Kiswahili na taaluma zake hususan fasihi na sarufi.
ii). Kutoa huduma za ukalimani kwa serikali na mashirika
iii). Kuratibu kazi za ukuzaji Kiswahili nchini na zile zinazofanyika nchi za nje.
iv). Kuchapisha majarida ya Kiswahili yatakayoongoza matumizi sahihi ya maneno na maendeleo yake.
v). Kuchunguza usahihi wa lugha ya Kiswahili inayotumika katika uandishi wa vitabu mbali mbali vinavyokusudiwa kutumika kufundishia shuleni na vyuoni kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu.
vi). Hujishughulisha na uthibitishaji wa tafsiri sanifuza isitilahi na kusimamia utafiti wa lugha ya Kiswahili.
vii). Kutoa ushauri kwa waandishi na wachapishaji kuhusu utumiaji wa Kiswahili fasaha na kuratibu maendeleo ya Kiswahili nchini.
Katika utekelezaji wa shughuli zake, baraza hilo limeanzisha idara tano za taaluma. Nazo ni:
Idara ya Uhariri na Uchapishaji.
Idara hii hujishughulisha na masuala mbali mbali ya uchapaji wa taarifa za BAKITA na majarida mengine.
Idara ya Lugha na Fasihi.
Idara hii husimamia matumizi sahihi ya Kiswahili sanifu katika vyombo vya habari na matumizi rasmi na kutoa ithibati ya vitabu vya Kiswahili vinavyokusudiwa kutumika katika elimu.
Idara ya Tafsiri na Ukalimani.
Idara hii hujishughulisha na kutoa huduma za tafsiri na ukalimani kwa lugha ya Kiswahili kwa mashirika,idara,wizara,balozi na watu binafsi.
Idara ya Istilahi na kamusi.
Hii inafanya kazi ya kufanya tafiti za isitilahi, kuandaa orodha ya isitilahi na kuandaa kamusi kwa matumizi ya asasi, shule na watu wa aina mbali mbali.
Idara ya Uhusiano
Idara hii inafanya kazi ya kutangaza kazi za shughuli za baraza kwa kutumia radio,magazete na majarida na kusimamia vipindi vya Kiswahili katika radio na televisheni, pamoja kuimarisha uhusiano baina ya vyombo vya ukuzaji Kiswahili kwa kuandaa warsha na semina.
MAFANIKIO YA BAKITA
. Bakita imeandaa isitalahi za taaluma mbali mbali kama vile za Fizkia, Kemia, Uchumi, Ufundi, Bunge , maktaba n.k
. Bakita inatoa majarida mbali mbali yanayohusu lugha ya Kiswahili kama vile lugha yetu tusome tuijue, jifunze Kiswahili uwafunze wengine , lugha ya kiswahili – fasihi na sarufi yaken.k
. Bakita huendesha vipindi mbali mbali vya Kiswahili katika radio Tanzania dar es sallam kama vile lugha yetu, ulimwengu wa Kiswahili, Kiswahili lugha ya taifa n. k
MATATIZO YA BAKITA.
4). TAASISI YA KISWHILI NA LUGHA ZA KIGENI. ( TAKILUKI ).
Taasisi hii iliundwa mwaka 1979 ikiwa chini ya Wizara ya Elimu na Mafuzo ya Amali Zanzibar.
Lengo kubwa ya kuanzishwa taasisi hii ni :Kusimamia na kuendeaha shughuli za ukuzaji wa kiswahli na lugha za kigeni kisiwani humo.
KAZI ZA TAKILUKI:
MAFANIKIO YA TAKILUKI.
Takiluki imepata mafanikio kadhaa yakiwemo haya yafutayo:
BAKIZA. ( BARAZA LA KISWAHILI ZANZIBAR ).
Ni chombo chengine ambacho kimesidia kukuza na kustawisha kugha ya Kiswahili visiwani Zanzibar. Baraza hili lilianzishwa mwaka 1983.
KAZI ZA BAKIZA.
CHAMA CHA KISWAHILI CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM
Chama hiki kilianzishwa mwaka 1970 kwa juhudi za mwanzo za wanafunzi walioingia chuo kikuu kusoma Kiswahili katika ngazi ya shahada ya kwanza.
Chombo hiki kilikuwa na madhumuni yafuatayo:
MAFANIKIO YA CHAMA HIKI.
TAASISI YA ELIMU.
Taassisi hii ilianzishwa mwaka 1966 na ilikuwa na kazi zifuatazo:
MAFANIKIO YA TAASISI HII.
TAASISI YA ELIMU YA WATU WAZIMA.
Taasisi hii ilianzishwa mwaka 1963. Kama chombo cha kuwasaidia wazelendo katika stadi za kusoma na kuandika ambao hawakupata fursa ya kupata elimu katika ngazi ya msingi na sekondari.
Baadhi ya mafanikio ya elimu ya watu wazima ni:
IDARA YA KISWAHILI – CHUO KIKUU DAR ES SALAAM
Idara hii ilianzishwa mwaka 1970 baada ya kuanzishwa chuo kikuu.
Kazi kubwa ya idara hii ilikuwa ni:
Mafanikio makubwa ya idara hii ni kuweza kutoa walimu wengi wenye shahada ya Kiswahili wanaofundisha mashuleni mashuleni na vyuoni,
Pia imeweza walimu wenye shahada ya pili , tatu na hata uprofesa wa lugha ya kiswahili.
CHAMA CHA KISWAHILI CHA AFRIKA.
Chama hiki kiliundwa katika semina ya kimataifa kuhusu usanifishaji wa isitilahi za Kiswahili iliyofanyika chuo kikuu dar es salaam mwaka 1978. Ikiwa na wajumbe tafauti waliotoka nchi za Kenya, Tanzania, msumbuji, na Zambia ikiwa na madhumuni yafuatayo:
Pia semina nyengine iliandaliwa tena mwaka 1983 na kuhudhuriwa na wajumbe kutoka Kenya, Rwanda, Comoro, Uganda, DRC, Zanzibar na kutoka radio mbali mbali kama vile India, BBC, RTD, Radio Rwanda n.k na waliazimia mambo yafuatayo:
MATATIZO YA CHAKA.
UWAVITA. ( Umoja wa waandishi wa vitabu Tanzania ).
Umoja huu ulianzishwa mwaka 1974 na ulikuwa na madhumuni yafuatayo:
TATHMINI YA MAENDELEO YA KISWAHILI BAADA YA UHURU.
Lugha ya Kiswahili baada ya uhuru imepata mafanikio kadhaa. Miongoni mwa mafanikio hayo ni:
Kiswahili kimeweza kuendelezwa kwa njia mbali mbali kama vile kufundisha kama somo moja wapo katika ngazi zote za elimu nchini, kufanyiwa utafiti, kusanifiwa na kutumika kama lugha kuu ya mawasiliano.
Kiswahii kimeweza kuenea hadi nje ya Tanzania katika mataifa mbali mbali na hata kufikia moja wapo lugha ya kimataifa na pia kuongezeka msamiati.
Kuendelea kujitokeza vyombo mbali mbali vya ukuzaji wa Kiswahili ndani na nje ya Tanzania ni mafanikio makubwa kwa upande wa lugha ya Kiswahili kwa sababu vyombo hivyo vimewea kuikuza lugha ya Kiswahili kwa njia mbali mbali.
Kuendelea kutumika lugha ya Kiswahili katika vyombo mbali mbali vya habari vya nje kama viel BBC. Deutchwelle,radio japani, sauti ya amerika na nyinginezo kumeifanya lugha ya Kiswahili kuwa miongoni mwa lugha mashuhuri duniani
CHANGAMOTO ZINAZOATHIRI MAENDELEO YA KISWAHILI.
Pamoja na mafanikio hayo ,zimekuwapo changamoto kadhaa zinazoathiri maendeleo ya Kiswahili. Baadhi ya changamoto hizo ni:
Upotwashwaji wa Kiswahili hutokea kwa namna kadhaa mfano ni wa uchanganyaji wa Kiswahili na kingereza na pia kutumia Kiswahili kwa maneno yasio yanifu na pia utumizi wa Kiswahili ulioathiriwa na sarufi ya lugha za kikabila hususan kimatamshi na kimuundo.
Tatizo la kutokithamini Kiswahili miongoni mwa wanajamii ni changamoto ya kuathiriwa na kasumba za ukoloni ambapo wanajamii huthamini Zaidi lugha za kigeni hususan kingereza.
Hii ni changamoto nyengine ambapo Kiswahili hakina uwiano wa kimatumizi katika nchi nzima, tofauti hizi zipo kutokana na jamii moja na nyingine kuathiriwa na lugha mama.
Juhudi za ukuzaji Kiswahili zinaonekana hazina mashiko kutokana na kuwepo idadi kubwa ya vyombo vya ukuzaji Kiswahili ambayo havina mshikamano wa pamoja kwani kila chombo kina malengo,sera, na mipango ya yake ya uendeshaji wa Kiswahili.
Uhaba wa wataalamu katika vyombo vya ukuzaji wa Kiswahili husababisha vyombo kutofanya na kutekeleza malengo kwa ufanisi.
Ni tatizo jengine linalokwanishwa maendeleo ya Kiswahili kwa kutotekelezwa kwa mpango wa kukitumia Kiswahili kama lugha ya kufundishia katika ngazi zote za elimu nchini, na hivyo kutoa mwanya hasa kwa lugha za kigeni kama vile kingereza kustawi zaidi na hivyo kuathiri nafasi ya Kiswahili katika jamii.
|