UKUTA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Taasisi za kukuza lugha (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=18) +--- Thread: UKUTA (/showthread.php?tid=1148) |
UKUTA - MwlMaeda - 09-06-2021 Hiki ni chama cha Usanifu wa Kiswahili na Mashairi . chama hiki kilianzishwa mwaka 1965 na mshairi Mathias Mnyapala kwa lengo la kukuza ushairi wa Kiswahili kwa ujumla.
Ukuta ilikuwa na malengo yafuatayo:
a). Kukuza lugha ya Kiswahili na ushairi kwa ujumla kwa njia ya kujishughulisha na kazi tafauti zinazohusiana na maendeleo ya Kiswahili na ushairi kama vile uhariri wa miswada ya Kiswahili, utunzi wa mashairi na uandishi wa vitabu na kutafsiri maandishi mbali mbali katika Kiswahili.
b). Kukuza utunzi wa ngonjera na kuhamasisha utunzi wa vitabu katika misingi yenye kuzingatia utamaduni wa Mtanzania.
Mafanikio ya UKUTA.
c). Imeweza kuundaa na kuendesha semina na makongamano ya Kiswahili na kutunga kazi za fasihi kwa kushirikiana na vyombo vingine.
d). UKUTA imeweza kuandika vitabu mbali mbali vya ushairi hususan vya ushairi, kama vile Ngonjera za ukuta ( cha kwanza na cha pili – 1968 ), Mashairi ya Azimio la Arusha – 1974 na Mashairi ya miaka kumi ya Azimio la Arusha – 1977.
e). Imeweza kutafsiri kwa Kiswahili maandishi mbali mbali . mfano , iliwza kutafisiri majina ya baadhi ya mitaa ya jiji la Dar – es – Salaam kama vile mtaa wa uhuru badala Independence Avenue na mtaa wa Sokoine badala ya Sokoine Drive.
Taasisi hii kihistoria ilianzishwa mwaka 1930 ikiwa kamati ya lugha ya lugha ya Afrika Mashariki na uatwala wa Waingereza , na mnamo mwaka mwaka 1964, ilipandishwa hadhi na kuhamishiwa katika chuo kikuu cha Dar –es – Salaam baada ya kuimarishwa kwa sheria ya Bunge ya mwaka 1964. Na mwaka 1970 kilipoanzishwa chuo kikuu cha Dar –es Salaam taasisi ilikuwa moja wapo wa asasi za utafiti wa chuo, ambapo mpaka leo asasi hii imekuwa ikifanya kazi chini ya Chuo Kikuu,
Mnamo mwaka 2009, taasisi hii ilibadili jina baada ya kuungana na Idara ya Kiswahili ya chuo na kujulikana kwa jina la Taasisi ya Taaluma za Kiswahili. ( TATAKI ).
Malengo ya TUKI ( TATAKI ).
i). Kuichunguza na kuiendeleza lugha ya Kiswahili katika fani zake zote ikizingatia mipango ya muda mrefu katika Jamhuri ya Muungao wa Tanzania, Afrika na mashariki na Katika chuo kikuu cha Dar es Salaam.
|