MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MASWALI YA KUJIPIMA (UTANGULIZI WA LUGHA NA ISUMU) NA MUONGOZO WA MAJIBU - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
MASWALI YA KUJIPIMA (UTANGULIZI WA LUGHA NA ISUMU) NA MUONGOZO WA MAJIBU - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Chuo (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=3)
+---- Forum: Shahada (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=20)
+----- Forum: Maswali na majibu (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=24)
+----- Thread: MASWALI YA KUJIPIMA (UTANGULIZI WA LUGHA NA ISUMU) NA MUONGOZO WA MAJIBU (/showthread.php?tid=1115)



MASWALI YA KUJIPIMA (UTANGULIZI WA LUGHA NA ISUMU) NA MUONGOZO WA MAJIBU - MwlMaeda - 09-02-2021

MASWALI YA KUJIPIMA (UTANGULIZI WA LUGHA NA ISUMU) NA MUONGOZO WA MAJIBU

1. (a) Fafanua sifa zozote tatu za lugha.
(b) Eleza malengo ya taaluma ya isimu.
© Tofautisha baina ya lugha ya binadamu na mawasiliano ya wanyama.
(d) Pambanua tanzu nne za isimu na ubainishe umuhimu wake.
2. “Isimu ni sayansi kwa sababu hufuata mbinu za kimsingi
za utafiti wa kisayansi.” Fafanua sifa nne kuu za uchambuzi wa kisayansi katika isimu.
3. Eleza jinsi kigezo cha namna ya kutamka kinavyotumika kuainisha konsonanti za lugha na utoe mifano ya uainishaji huo katika Kiswahili.
4. Ingawa fonetiki na fonolojia zinajishughulisha na uchunguzi wa lugha, kila taaluma ina mwelekeo wake tofauti katika uchunguzi na uchambuzi. Thibitisha.
5. Toa maelezo mafupi kuhusu matawi yafuatayo ya isimu huku ukieleza misingi ya uchunguzi ya kila tawi.
a. Isimu fafanuzi
b. Isimu Historia
c. Isimu Linganishi
d. Isimu-jamii
MWONGOZO WA KUTAHINI
1. (a) Sifa za lugha:
  •       Lugha
    ni mfumo
  •       Lugha
    ni ishara
  •       Lugha
    ni nasibu
  •       Lugha
    ni sauti
  •       Lugha
    ni mawasiliano
  •       Lugha
    ni sifa ya binadamu
(b) Malengo ya taaluma ya Isimu
  •  Kuchambua na kueleza maarifa au umilisi wa mzawa wa lugha kuhusu lugha yake.
  • Kuunda nadharia, nadharia husaidia kuonesha ruwaza zilizomo katika lugha na jinsi inavyofanya kazi.
  • Kubainisha mbinu za kisayansi za kuchambua lugha ili matokeo yaweze kukubalika na yawe yamejengwa kwa misingi thabiti.
 © Tofauti
kati ya lugha ya binadamu na mawasiliano ya wanyama:
  • Lugha ya binadamu ni ishara ya sauti ila wanyama hutumia milio tu
  • Binadamu ana uwezo wa kujifunza lugha iliyomo katika mazingira yake, wanyama hawana uwezo wa kujifunza lugha
  • Binadamu ana uwezo wa kuelezea mambo yaliyopo, layiyopita na yatakayokuja, wanyama hawana uwezo huo, ila nyuki kwa kiwango kidogo sana
  • Binadamu akilelewa katika mazingira ombwe yasiyo na lugha,
    hatakuwa na lugha yoyote ila mnyama akilelewa katika mazingira kama hayo atatoa milio ya aila yake
  • Binadamu harithi lugha bali hubwia/ hupata lugha ila wanyama hurithi milio ya aila yao
(d) i. Fonetiki
Fonetiki ni kiwango cha isimu kinachojishughulisha na uchunguzi na uchambuzi wa taratibu zote zinazohusiana na utoaji, utamkaji,
usafirishaji, usikiaji na ufasili wa sauti za lugha za binadamu kwa jumla. – Husaidia kuimarisha matamsi bora ya sauti na kwa hivyo kuimarisha matumizi ya lugha fasaha.
ii. Fonolojia
Fonolojia ni kiwango cha isimu ambacho hujishughulisha na uchunguzi, uchambuzi na uanishaji wa sauti pambanuzi ambazo hutumika katika mifumo mbalimbali ya sauti za lugha za binadamu. – Fonolojia huweka misingi ya jinsi lugha tofauti zinavyotumia sauti chache tu ili kuunda maneno.
iii. Mofolojia
Mofolojia ni taaluma inayoshughulikia vipashio vya lugha na mpangilio wake katika uundaji wa maneno. Vipashio hivyo vya lugha huitwa mofimu.
– Mofolojia huchunguza jinsi mofimu zinavyofuatana kwa utaratibu unaokubalika ili kuunda maneno.
iv. Sintaksia
Ni taaluma ya isimu inayochunguza na kuchambua jinsi maneno hupangwa ili kuunda sentensi za lugha kwa kufuata kanuni za sarufi katika lugha husika. – Sintaksia husaidia kuainisha miundo mbalimbali ya lugha na jinsi kanuni za sarufi hufanya kazi katika miundo mbalimbali ya lugha.
v. Semantiki
Ni taaluma inayojishughulisha na muundo wa maana katika lugha ya binadamu. – Dhima ya lugha ni mawasiliano, hivyo basi semantiki huchunguza jinsi maneno hupata na kuwasilisha maana ili kuwezesha mawasiliano
2. Zipo sifa nne kuu za uchambuzi wowote wa kisayansi. Sifa hizo ni pamoja na:
a) Uwazi na Ukamilifu
Dhana hii ina maana kuwa masuala katika isimu huelezwa kwa udhahiri usio na utata. Hoja huelezwa bila shaka yoyote kimaana. Ni sifa inayomtaka mwanaisimu kujiwekea lengo la kupima kwa uangalifu kila analofanya na kuhakikisha kuwa hoja zake zote anazotoa ili kutegemeza nadharia zake au mahitimisho yake ziko
wazi na zinatokana na utafiti wake. Wakati uchunguzi unapofanywa huwa kuna machukulio. Machukulio haya hubainishwa wazi.
Kwa mfano, mwanaisimu anaweza kuchunguza jinsi watu hujifunza lugha za pili na matatizo ambayo huwakumba. Machukulio ya utafiti kama huu ni kuwa hawa watu wana bongo imara na razini. Hili inabidi mchunguzi aweze kulibainisha.
b) Utaratibu/Upangilifu
Utaratibu ni kufanya mambo kwa mpangilio mzuri wenye kubainika. Utaratibu unaweza kuhusisha wakati, idadi, umuhimu na hata ukubwa. Kwa mujibu wa sifa hii, hoja za kisayansi zinapaswa kupangwa vizuri. Taaluma yoyote ya kisayansi hufuata utaratibu maalumu na mambo yake huendeshwa hatua kwa hatua. Wanaisimu huichunguza lugha kwa utaratibu maalumu, si
kiholela.Wanaisimu wamejaribu kuweka mpangilio wa kufuata katika uchunguzi wa lugha. Mpangilio huu hurahisisha kazi inayowakabili. Mpangilio huu unajitokeza katika hatua zifuatazo:
a) Kutambua tatizo linalohitaji uchunguzi
b) Kuunda nadharia tete
c) Kuchagua nadharia ya kuongoza utafiti
d) Kukusanya data
e) Kuchanganua data
c) Urazini/Uhoromo/Uhakikifu
Sifa hii pia inajulikana kama utonafsi au kutopendelea. Huku ni kutazama mambo yalivyo bila kushawishiwa na hisia. Katika kuzingatia sifa hii, mwanasayansi anapaswa kuhakikisha kuwa yale anayoyasema, pamoja na mahitimisho anayoyafikia, yanatokana na data zilizo wazi na ambazo zinaweza kuchunguzika. Tamko lolote la
kisayansi lazima liweze kuthibitishwa na hoja. Umuhimu wa sifa hii ni kuhakikisha kwamba wanaisimu hawatoi matamko ya juujuu, ambayo hayawezi kuthibitishwa.
d) Iktisadi
Iktisadi ni sifa ya sayansi inayohitaji uchanganuzi ulenge katika kutumia vipashio vichache zaidi kadri iwezekanavyo. Inaeleza kwamba taarifa fupi ni bora kuliko sentensi ndefu ndefu. Imekuwa
kawaida kwa sayansi kutumia fomula na kanuni zilizoandikwa kwa ufupi ili kueleza mambo kwa usahihi bila kutumia maneno mengi. Kwa mfano katika somo la Kemia fomula H2O inarejelea ‘maji’. Tutatoa mfano mmoja kutoka kwa fonolojia na sintaksia.
/z/ au /v/ katika mazingira ya kutangulia /i/. Kwa mfano, iba …….*mwibi ….. mwizi / mwivi.
a) Sintaksia
Juma alikula mkate wa mtoto.
S ……….. KN + KT
Maelezo yake: sentensi hii imeundwa kwa Kundi Nomino
(KN) na Kundi Tenzi (KT).
3. Kwa kutumia kigezo cha namna ya kutamka, konsonanti huainishwa katika
makundi yafuatayo:
a) Vipasuo/Vizuiwa (Stops/Plosives)
b) Nazali/Ving’ong’o (Nasals)
c) Vikwamizwa/Vikwaruzo (Fricatives)
d) Vipasuo-kwamizwa/Vizuiwa-kwamizwa (Affricates)
e) Vitambaza (Laterals)
f) Vimadende (Trills)
a) Vipasuo/Vizuiwa
Sauti hizi zinapotamkwa kwanza hewa hutoka mapafuni, husukumwa nje kwa nguvu na huzuiwa kabisa kabla ya kuachiliwa kwa gafla na kutoa sauti ambayo hufanana na sauti isikikayo wakati
kitu kinapolipuka. Vizuiwa katika Kiswahili ni [p],
, [t], [d], [k] na [g].
b) Nazali/Ving’ong’o
Nazali ni aina ya konsonanti ambazo hutamkwa kwa kukishusha kimio kwa namna ambayo kiasi kikubwa cha hewa kutoka mapafuni huelekezwa kupitia kwenye chemba cha pua. Nazali za Kiswahili ni pamoja na [m], [n], [ɲ] na [ŋ].
c) Vikwamizwa/Vikwaruzo
Hutamkwa wakati alasauti zinapokuwa zimekaribiana kiasi cha kutosha kuweza kusikia mkwaruzo unaotokea wakati hewa inapopita kati ya ala hizo. Vikwamizwa vilivyopo katika Kiswahili ni [ƒ], [v], [θ], [ð], [s], [z], [∫], [χ], [ɣ] na [h].
d) Vipasuo-kwamizwa/Vizuiwa-kwamizwa
Konsonanti hizi zinapotamkwa, hewa husukumwa nje kwa nguvu, huzuiwa halafu nafasi ndogo huachwa ili hewa ipite ikiwa na mkwaruzo. Vizuiwa-kwamiza katika Kiswahili ni [t∫] na [ŋɟ].
e) Vitambaza
Hutamkwa kwa hewa kusukumwa nje, kuzuiwa na kuruhusiwa kupita pembeni mwa kizuizi bila mkwaruzo mkubwa sana. Kitambaza cha pekee katika Kiswahili ni [l].
f) Vimadende
Hutamkwa ncha ya ulimi ikiwa imeugusa ufizi lakini kutokana na nguvu ya hewa inayopita kati ya ncha ya ulimi na ufizi, ncha ya ulimi hupigapiga kwa harakaharaka kwenye ufizi. Katika Kiswahili kuna kimadende kimoja tu, nacho ni [r].
Uhusiano kati ya fonetiki na fonolojia unatokana na ukweli kwamba taaluma zote mbili zinajishughulisha na uchunguzi na uchambuzi unaohusu lugha za binadamu. Hata hivyo, kila taaluma ina mwelekeo wake tofauti katika uchunguzi na uchambuzi huo.
4. Tofauti kati ya Fonetiki na Fonolojia
 
[Image: SAM_1547.JPG]
5. Matawi ya Isimu:
 
a) Isimu Fafanuzi/Elezi
Tawi hili linazingatia umuhimu wa kuchambua au kufafanua vipengele vya lugha jinsi vilivyo. Huchunguza jinsi lugha inavyozungumzwa wakati fulani na watu fulani. Kimsingi, isimu
fafanuzi inahusika na lugha wakati huohuo wala sio uliopita au ujao. Tawi hili ndilo shina kubwa la isimu. Isimu fafanuzi haitilii mkazo mabadiliko yaliyotokea katika lugha hata kama mabadiliko haya yapo. Katika utanzu huu ndipo tunachambua muundo wa sauti za lugha, muundo wa maneno, muundo wa sentensi, na hata maana za tungo za lugha.
b) Isimu Historia
Isimu historia ni miongoni mwa matawi makongwe zaidi. Tawi hili ndilo linashughulikia uchunguzi wa maendeleo na mabadiliko ya lugha kiwakati kutoka kipindi kimoja cha kihistoria hadi kingine, sababu na matokeo ya mabadiliko hayo. Isimu historia hudhihirisha mabadiliko ya sauti, maumbo ya maneno, sentensi, na maana za maneno kihistoria.
Isimu historia ni uchunguzi wa mabadiliko ya lugha katika mapito ya nyakati. Inaangaza jinsi lugha inavyobadilika katika vipindi mbalimbali, sababu za mabadiliko hayo na athari zake katika lugha hiyohiyo na lugha nyinginezo. Tawi hili pia huangalia hatua mbalimbali ilizopitia lugha katika kukua kwake.
c) Isimu Linganishi
Hili ni tawi la isimu ambalo linafanya uchunguzi wa lugha mbalimbali ili kuzilinganisha na kuzilinganua. Wanaisimu huchunguza lugha katika viwango vyote vya fonolojia, mofolojia,
sintaksia na semantiki ili kuonesha na kueleza jinsi lugha hizo zinavyofanana au kutofautiana. Isimu Linganishi ndiyo imewezesha kubainisha makundi mbalimbali ya lugha. Kwa mfano, familia za lugha kama vile lugha za ulaya na za kihindi na makundi mbalimbali ya lugha za kiafrika. Wanaisimu wanapozilinganisha lugha mbalimbali, hufanikiwa kuunda lugha mame ya lugha hizo. Kutokana na hiyo lugha mame mwanaisimu hubainisha lugha hizo na uhusiano wa kinasaba na kuonesha jinsi lugha hizo zinavyotofautiana.
d) Isimujamii
Hili ni tawi la isimu linalochunguza uhusiano uliopo baina ya lugha na watumiaji wake au jamii. Baadhi ya mambo muhimu ambayo huchunguzwa ni pamoja na sera za lugha, lugha sanifu, usanifishaji, lahaja, rejesta au sajili. Maswali muhimu yanayojibiwa katika utanzu huu ni pamoja na: nani anasema nini, kwa nani au na nani, wakati gani, kuhusu nini. Wanaisimujamii huamini kwamba umuhimu wa lugha upo katika matumizi yake. Hii ndiyo sababu wanachunguza lugha katika miktadha yake ya jamii.