SWALI: ELEZA KWA MIFANO KIIMA NA KIARIFU NA VIJENZI VYAKE - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Chuo (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=3) +---- Forum: Shahada (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=20) +----- Forum: Maswali na majibu (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=24) +----- Thread: SWALI: ELEZA KWA MIFANO KIIMA NA KIARIFU NA VIJENZI VYAKE (/showthread.php?tid=1112) |
SWALI: ELEZA KWA MIFANO KIIMA NA KIARIFU NA VIJENZI VYAKE - MwlMaeda - 09-02-2021 SWALI: Eleza kwa mifano Kiima na Kiarifu na vijenzi vyake. James, J na Faustino, M (2014) wanasema Kiima ni kipashio ambacho, aghalabu hutokea kabla ya kitenzi. Kipashio hiki hutaja mtenda au mtendwa wa jambo linaloelezwa kwenye tungo. Hao hao Oxford wanasema Kiarifu ni sehemu kkatika sentensi inayotoa taarifa kuhusiana na kiima. Ni sehemu inayoeleza kiima kimetenda nini, kimetendwa nini au kikoje.
Mdee, J. S (1999) anaeleza kuwa Kiima ni sehemu ya sentensi ambayo hutaja mtenda wa jambo linaloelezwa. Kiima aghalabu hutokea kushoto kwa kitenzi katika tungo. Mdee anaeleza Kiarifu kuwa ni sehemu inayojazwa na neno au maneno yanayoarifu tendo. Kiarifu ndiyo sehemu muhimu zaidi katika tungo ambayo wakati mwingine huweza kusimama pekee bila kiima kwani huchukua viambishi viashiria kiima.
Vipashio vya Kiima
Mdee anafafanua kuwa Kiima kinaweza kujengwa na vipashio mbalimbali kama vifuatavyo:
NominoMfano: Mtoto anasoma Juma anakimbia Kiwakilishi Mfano: Yeye haishi hapa Sisi tutaondoka pamoja Yule hataki kuondoka Wangu wanifuate Nomino na Kivumishi Mfano: Watoto wote wameondoka Wasichana wazuri wamewasili Kitabu kidogo kuliko vyote kimeuzwa Nomino na kishazi tegemezi kivumishi Mfano: Mtoto aliyeingia hapa amefiwa Kisu kilichopotea kimeonekana Kalamu iliyoisha wino imetupwa Kitenzi nomino na Kivumishi Mfano: Kuimba kwenu kulitufurahisha Kuja kwao kulitutia faraja Vipashio vya Kiarifu
Kwa mujibu wa James Mdee Kiarifu kinajengwa na prediketa, kijalizo au chagizo kama ifuatavy:
Prediketa
Hii ni sehemu ya sentensi ambayo hujazwa na aina yoyote ya kitenzi (kishirikishi, kisaidizi au kitenzi kikuu). Prediketa ndiyo sehemu muhimu ambayo sentensi inapaswa kuwa nayo.
Mfano:
Juma ni mwananguAli anasoma kitabu Maria alikuwa anapika chakula jikoni Asha yupo chumbani Kijalizo Hii ni sehemu ya sentensi ambayo hujazwa na nomino au kikundi nomino katika kiarifu. Nomino au kikundi nomino hiki huwakilisha mtendwa, mtendea au kitendea. Kijalizo hufuata kitenzi katika sentensi iliyo nacho. Kijalizo ni kipashio kisichojitokeza katika kila sentensi. Hutokea katika sentensi yenye kitenzi kinachohitaji kukamilishwa na nomino au kikundi nomino. Mfano: Baba analima shamba Watalii wanaangalia nyumba mpya zilizojengwa Malima ni mwalimu mpole Nimempatia rafiki yangu kalamu Chagizo Hii ni sehemu ya sentensi inayojazwa na kielezi au kikundi kielezi cha aina yoyote kama vile vielezi vya idadi, namna, wakati au mahali kitendo kilipofanyika. Chagizo huweza kutokea mara baada ya kitenzi au kijalizo kutegemeana na muundo wa sentensi inayohusika, na vipashio vilivyomo. Mfano: Mama anasoma barua kimya Mama anasoma kimya Tutaondoka alfajiri na mapema Watoto wanacheza uwanjani Nimeondoa vitabu vyote mezani Kwa ujumla Kiima na Kiarifu ni istilahi za sarufi mapokeo ambayo huitazama sentensi na vipashio vyake kiuamilifu (kikazi). Kwa wanamapokeo kila istilahi katika tungo ina kazi maalumu ambayo huitambulisha istilahi husika. MAREJELEO
James, J na Faustino, M (2014) Kiswahili Kidato cha Tano na Sita. Oxford University Press. Dar es Salaam.
James, J. S (1999) Sarufi ya Kiswahili: Sekondari na Vyuo. DUP. Dar es Salaam.
|