OSW 123/133: FASIHI YA KISWAHILI NADHARIA NA UHAKIKI - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Chuo (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=3) +---- Forum: Shahada (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=20) +----- Forum: Maswali na majibu (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=24) +----- Thread: OSW 123/133: FASIHI YA KISWAHILI NADHARIA NA UHAKIKI (/showthread.php?tid=1107) |
OSW 123/133: FASIHI YA KISWAHILI NADHARIA NA UHAKIKI - MwlMaeda - 09-02-2021 SWALI: 3 Andika kumhusu mwalimu maarufu wa uhakiki wa kazi za fasihi nchini Tanzania.
JIBU
Uhakiki wa kazi za
fasihi ni taaluma ambayo nchini Tanzania muasisi wake ni mwalimu wa walimu, gwiji wa uhakiki almaarufu T.S.Y Sengo. Umaarufu wa mwalimu huyu upo katika kufundisha wahakiki wengi lakini pia katika kuweka misingi ya nadhariya za kuhakikia kazi za fasihi. Uhakiki uliofanywa
katika HISI ZETU unatoa mwanga katika kazi ya uhakiki licha ya baadhi ya wanafunzi wake kutaka kuleta hadithi za sikio kupita kichwa kwa kumkosoa mwalimu mkongwe kuwa amekosea kuzungumzia hisi badala ya hisiya ingawa hawakufua dafu. Umaarufu wa mwalimu wa
uhakiki unajidhihirisha pia katika kitabu chake cha SENGO NA FASIHI ZA KINCHI ambamo anatoa nadhariya za kumuongoza mhakiki yeyote wa kazi ya fasihi ili kuifanya kazi ya uhakiki kuwa taaluma yenye misingi thabiti halikadhalika anaonesha maana halisi ya uhakiki kwa kuchambua diwani ya Wasakatonge iliyoandikwa na M.S. Khatib kwa kukosoa pale alipokosea katika utunzi na kukiuka nadharia za utunzi kama vile hadhira ya uhalisia pamoja na ile ya Kiislamu. Mwalimu Sengo pia ni
maarufu katika utunzi na umaarufu huo unajidhihirisha katika diwani yake ya TUNGIZI ZA MNYAGATWA ambapo amesheheni mashairi yenye kufikirisha, lugha nzito yenye kuthibitisha hasa uwezo mkubwa alionao katika kuimudu lugha. Kwa ujumla mwalimu
Sengo ni mtaalamu mbobezi wa taaluma ya uhakiki wa kazi ya fasihi ambaye mchango wake haupaswi kupuuzwa wala kuchukuliwa kirahisi na mtu yeyote. |