KISWAHILI 1 : JINSI YA KUJIBU MASWALI YA SEHEMU C : UTUNGAJI - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Sekondari (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=4) +---- Forum: Kidato cha tano na sita (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=44) +----- Forum: Maswali na majibu (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=47) +----- Thread: KISWAHILI 1 : JINSI YA KUJIBU MASWALI YA SEHEMU C : UTUNGAJI (/showthread.php?tid=1101) |
KISWAHILI 1 : JINSI YA KUJIBU MASWALI YA SEHEMU C : UTUNGAJI - MwlMaeda - 09-02-2021 KISWAHILI 1 : JINSI YA KUJIBU MASWALI YA SEHEMU C : UTUNGAJI SWALI:
Wewe ni mhitimu wa fani ya elimu na umekusudia kuomba kazi Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI). Andika wasifu kazi utakaouambatanisha kwenye barua yako ya kuombea kazi.
MAJIBU
Mfano:
Taarifa binafsi
Majina: TAFUTA MAISHA USICHOKE
Utaifa: MTANZANIA
Mahali pa kuzaliwa: ARUSHA
Tarehe ya kuzaliwa: 26/11/2017
Jinsi: ME
Hali ya Ndoa: SIJAOA
Anwani ya Posta:
MBEZI BEACH
S.L.P 4507
DAR ES SALAAM
Simu: 0717104507
Barua pepe: mwalimwakiswahili@gmail.com
Sifa za kitaaluma
2006-2009: Shahada ya Sanaa katika Elimu. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
2004-2006: Cheti cha Elimu ya sekondari ya juu. NECTA
2000-2003: Cheti cha Elimu ya sekondari ya kawaida. NECTA
1993-1999: Elimu ya Msingi. Shule ya Msingi Mto wa Mbu
Uzoefu na historia ya kuajiriwa
2013-2015: Mwandishi wa Habari za Mazingira, Mwananchi Communications
Ltd
Ujuzi na weledi
Katika sehemu hii onesha aina ya ujuzi na weledi uliowahi kuupata kupitia warsha, semina na makongamano yalivyokusaidia kuongeza ujuzi mwepesi unaoweza kukusaidia kuzalisha, kukuza, kubuni, kuanzisha, kusababisha, kubadili, kuchangia mabadiliko na kuwezesha.
Onesha mahali, mwaka, shughuli husika na malengo yake kwa mtiririko wa kuanzia hivi karibuni mpaka yale ya zamani.
Mapendeleo
Ninapendelea kuogelea, kusoma magazeti na habari habari mbalimbali za kijamii, kusogoa kwenye mitandao ya kijamii.
Tuzo au heshima
Mwajiri huvutiwa na mtu anayeweza kuonyesha namna jitihada zake zilivyotambuliwa na wengine. Onesha namna bidii, na ari yako ya kazi ilivyowahi kutambuliwa katika ajira zilizopita.
Siyo lazima iwe kazini tu, inawezekana kuwa katika masomo, lakini ziwe tofauti na zile tuzo za kitaaluma moja kwa moja.
Maneno kama, nilishinda, nilituzwa na nilitambuliwa, kwa sababu ya shughuli, majukumu, jitihada zilizowahi kufanywa, yanakuongezea nafasi ya kukubalika.
Orodha ya wadhamini
MAJURA KAMAZI
S.L.P 1020
TANGA
SIMU: 0717104507
CHARLES MAZIKU
S.L.P 1045
DAR ES SALAAM
0684104507
TAMKO
Mimi…………………ninatamka kuwa taarifa zilizotolewa kwenye wasifu kazi huu ni zangu na sahihi kwa mujibu wa uelewa wangu.
|