TOFAUTI KATI YA TENZI NA MASHAIRI - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi andishi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=7) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=54) +---- Thread: TOFAUTI KATI YA TENZI NA MASHAIRI (/showthread.php?tid=11) |
TOFAUTI KATI YA TENZI NA MASHAIRI - MwlMaeda - 06-14-2021 Tenzi na mashairi hutofautiana hasa katika vipengele muhimu vifuatavyo: – 1. MUUNDO Tenzi hutumia muundo wa tarbia katika beti zake ambapo mashairi yanauhuru wa kutumia miundo mingine tofauti kama vile tathilitha, takhmisa. 2. UREFU Tenzi kwa kawaida ni ndefu kwa vile hutoka zikiwa katika mtindo wa usimulizi na hivyo kuwa na beti nyingi sana ili kukamilisha usimulizi wa kisa ambapo mashairi kwa kawaida hutumia beti chache. 3. VINA Tenzi zina vina vya mwisho tu, hazina vina vya kati ambapo mashairi yana vina vya kati na vya mwisho. 4. UREFU WA MSTARI Tenzi mistari yake ni mifupi, haigawanyiki katika nusu ya kwanza na ya pili. Mashairi mistari yake ni mirefu na hugawanyika mara mbili, nusu ya kwanza na nusu ya pili huitwa vipande. 5. IDADI YA MIZANI Tenzi katika mistari yake huwa na mizani isiyozidi kumi na mbili, mashairi huwa na mizani 16 katika mistari yake. 6. KITUO Kituo cha utenzi hubadilikabadilika kutoka ubeti mmoja hadi mwingine, kituo cha shairi kinaweza kubadilika au kutobadilika. |