MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

SHAIRI: NAACHAJE? - Printable Version
|
SHAIRI: NAACHAJE? - Printable Version
+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6)
+---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50)
+---- Thread: SHAIRI: NAACHAJE? (/showthread.php?tid=1094)
|
SHAIRI: NAACHAJE? - John John - 09-01-2021
NAACHAJE?
Moyoni ameingia, naachaje kumpenda?
Mahaba anayajua, naahidi kumlinda,
Machoni anavutia, kwa mwingine sitoenda,
Naachaje kumpenda, mrembo aloumbika?
Mfano wake siuoni, uzuri alojaliwa,
Ngozi yake ya laini, kipenzi ameumbiwa,
Mwingine sitotamani, ya nini kujisumbua?
Naachaje kumpenda, mrembo aloumbika?
Anipatia furaha, daima nachekelea,
Vi maneno vya mzaha, hachoki kuniambia,
Si mjuzi wa karaha, mrembo ametulia,
Naachaje kumpenda, mrembo alojmbika?
Naahidi kumlinda, wezi wasimkwapue,
Wakafanya nikakonda, rahaye niijutie,
Nikikosa langu tunda, nitaghafirika mie,
Naachaje kumpenda, mrembo aloumbika?
RE: SHAIRI: NAACHAJE? - MwlMaeda - 09-01-2021
Kongole sana kwa umahiri wa mashairi. Usisahau kuweka taarifa zako chini ya shairi ili kuonesha kuwa mtunzi ni wewe
RE: SHAIRI: NAACHAJE? - John John - 09-01-2021
(09-01-2021, 02:03 PM)MwlMaeda Wrote: Kongole sana kwa umahiri wa mashairi. Usisahau kuweka taarifa zako chini ya shairi ili kuonesha kuwa mtunzi ni wewe
Ahsante sana kwa kunikumbusha ndugu yangu
|