VITENDAWILI NA MAANA ZAKE - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Semi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=49) +---- Thread: VITENDAWILI NA MAANA ZAKE (/showthread.php?tid=1059) |
VITENDAWILI NA MAANA ZAKE - MwlMaeda - 08-29-2021 VITENDAWILI NA MAANA ZAKE A 1. Adui lakini po pote uendako yuko nawe. Inzi 2. Afahamu kuchora lakini hajui achoracho. Konokono 3. Afuma hana mshale. Nungunungu 4. Ajenga ingawa hana mikono. Ndege 5. Ajifungua na kujifunika. Mwavuli 6. Akitokea watu wote humwona. Jua 7. Akitokea watu wote hunungunika na kuwa na huzuni. Ugonjwa 8. Akivaa nguo hapendezi, akiwa uchi apendeza. Mgomba 9. Alipita mtu ana bunda la mshale. Mkindu 10. Alipita mtu mwenye kibandiko cha nguo. Inzi 11. Aliwa, yuala; ala, aliwa. Papa 12. Amchukuapo hamrudishi. Kaburi 13. Amefunika kote kwa blanketi lake jeusi. Giza 14. Amefunua jicho jekundu. Jua 15. Ameingia shimoni akiwa uchi, akatoka amevaa nguo nzuri. Mbegu 16. Amejitwika mzigo mkubwa kuliko yeye mwenyewe. Konokono/Koa 17. Amekaa kimya na watoto wamemzunguka pande zote. Mgomba 18. Amekula ncha mbili. Wali 19. Amevaa joho kubwa kuliko yeye mwenyewe. Kaburi 20. Anakuangalia tu wala halali au kutembea. Picha 21. Anakula kila siku lakini hashibi na hatashiba. Mchanga 22. Anakula lakini hajashiba na hatashiba milele. Ardhi 23. Anakula lakini hashibi. Mauti 24. Anapendwa sana ingawaje ni mkali sana. Moto 25. Anatoka kutembea, anakuja nyumbani anamwambia mama, ‘Nieleke’. Kitanda 26. Ashona mikeka wala hailali. Maboga 27. Askari wangu wote wamevaa kofia upande. Majani 28. Askari wangu wote wamevaa mavazi meusi. Chunguchungu 29. Asubuhi atembea kwa miguu mine, adhuhuri kwa miwili. Fedha 30. Atapanya mbegu nyingi sana lakini hazioti. Mvua 31. Atolewapo nje hufa. Samaki B 32. Baba alinipa mfupa, nikautunza ukawa fahali. Muwa 33. Baba ameweka mkuki nje nikashindwa kuukwea, mdogo wangu akaukwea. Sisimizi 34. Babako akojoapo hunung’unika. Mawingu 35. Babu amefunga ushanga shingoni. Mtama/Nazi 36. Babu anakula ng’ombe, analea fupa linakuwa ng’ombe. Muwa 37. Babu hupiga kelele akojoapo. Mvua 38. Babu mkubwa ameangushwa na babu mdogo. Mti na shoka 39. Babu, nyanya, mjomba, mama, baba na watoto, mna safari ya wapi? Siafu 40. Bak bandika, bak bandua. Nyayo 41. Bawabu mmoja tu asiyeogopa chochote duniani. Mlango 42. Bibi kikongwe apepesa ufuta. Kope za macho 43. Bibi yake hutandikwa kila siku, lakini hatoroMoyoKinu cha kutwangia C 44. Chakula kikuu cha mtoto. Usingizi 45. Cha ndani hakitoki nje, cha nje hakiingii ndani. Nyama na mfupa 46. Chang’aa chapendeza, lakini hakifikiwi. Jua 47. Chatembea na hakijapata kupumzika hata nukta moja. Mwezi/Jua 48. Cheupe chavunjika manjano yatokea. Yai 49. Chumba change kina ukuta niondoa na kuusimika nitakapo. Pazia 50. Chungu change cha udongo hakipasuki kikianguka. Mjusi/Panya 51. Chungu kikubwa sana chenye kifuniko kikubwa sana. Dunia na mbingu D 52. Dada yangu akitoka kwao harudi kamwe. Jani likwanyukapo 53. Dada yangu kaoga nusu. Jiwe mtoni 54. Drrrrrh1 Ng’ambo. Daraja la buibui 55. Dume wangu amelilia machungani. Radi F 56. Fahali wa ng’ombe na mbuzi wadogo machungani. Mwezi na nyota angani 57. Fika umwone umpendaye. Kioo 58. Fuko kajifukia, mkia kaacha nje. Kata mtungini 59. Funga mizigo twende Kongo. Mikia ya mbwa H 60. Hachelewi wala hakosei safari zake. Jua 61. Haina miguu wala mikono, lakini, yabeba magogo. Maji 62. Hakihitaji maji, wala udongo, wala chakula; lakini chamea. Nywele 63. Hakionekani wala hakishikiki. Hewa 64. Hakisimami, na kikisimama msiba. Moyo 65. Hakuchi wala hakuchwi. Kula 66. Halemewi wala hachoki kubeba. Ardhi 67. Hamwogopi mtu yeyote. Njaa 68. Hana mizizi, nimemkata mara nyingi lakini haachi kukua. Ukucha 69. Haoni kinyaa. Mvua 70. Hapo nje panapita mtu mwenye miguu mirefu. Mvua 71. Hasemi, na akisema hatasahaulika. Kalamu 72. Hasimamishwi akiwa na ghadhabu. Upepo 73. Hata inyeshe namna gani haifiki humu. Kwapani 74. Hata jua likiwaka namna gani hakauki wala kupata joto. Pua ya mbwa 75. Hata Mzungu ameshindwa. Mauti 76. Hauchagui chifu wala jumbe. Utelezi 77. Hausimiki hausimami. Mkufu 78. Hawa wanaingia hawa wanatoka. Nyuki mzingani 79. Hesabu haihesabiki. Nyota 80. Huitumia kila siku lakini haiishi. Miguu 81. Huku kutamu, huku kutamu, katikati uchungu. Jua 82. Huku unasikia ‘pa’ Huku unasikia ‘pa! Mkia wa kondoo 83. Hula lakini hashibi. Sindano 84. Hulala tulalapo, huamka tuamkapo. Jua 85. Humu mwetu tuko wanne tu, ukimwona wa tano mwue. Matendegu ya kitanda 86. Huna macho lakini wakamata wanyama. Ndoana 87. Hupanda mtini na mwenye kichaa wake. Kivuli 88. Hutembea watatu. Mafiga 89. Hutoka upesi sana lakini hasalimu. Kuku 90. Huwafanya watu wote walie. Moshi 91. Huwezi kukalia alipokalia msichana wangu mweusi. Chungu jikoni 92. Huzikwa mmoja, hufufuka mmoja, huzeeka wengi. Mbegu na matunda I 93. Inaonekana mara mbili katika dakika moja na mara moja tu katika mwaka. Herufi "K" 94. Ini la ng’ombe huliwa hata na walioko mbali. Kifo J 95. Jembe la Wangoni haliishi. Miguu/Nyayo 96. Je, unaweza, kukua ukampita mzee wako? Nywele kichwani 97. Jiwe litoalo maji. Macho K 98. Kaburi la mfalme lina milango miwili. Kata ya kuchukulia Maji kichwani 99. Kaka yangu anapanda darini na fimbo nyuma. Paka na mkia wake 100. Kama kingekuwa mkuki, ungekuta kimekwisha kuua wote. Kizingiti cha mlango 101. Kama unapenda, mbona usile? Ulimi 102. Kanipa ngozi nikapikia, kanipa nyama nikala, kanipa mchuzi nikanywa, kanipa mfupa nikautumia. Nazi 103. Kapanda mti pamoja na uchawi wake. Tumbaku inaponuswa puani 104. Kidimbwi kimezungukwa na majani. Macho 105. Kikioza hutumiwa, kikiwa kichungu hakitumiwa. Maziwa 106. Kila linapofika kwetu hutanguliza makelele. Mvua 107. Kila mtu atapitia malango huo. Kifo 108. Kila mtu hata mfalme huheshimu akipita. Mlango 109. Kila siku hupita njia hiyo hiyo bali arudipo hatumwoni. Jua 110. Kileee! Hiki hapa. Kivuli 111. Kilimsimamisha chifu njiani. Chawa 112. Kina mikono na uso lakini hakina uhai. Saa 113. Kinaniita lakini sikioni. Mwangwi 114. Kisima cha Bimpai kina nyoka muwai, ndiye fisadi wa maji. Taa ya utambi 115. Kisima kidogo kimejaa changarawe. Kinywa na meno 116. Kitendawili change ukikitambua nitakupa hirizi. Mimba 117. Kiti cha dhahabu hakikaliwi na watu. Moto 118. Kiti cha Sulatni hukaliwa na mwenyewe. Kuku aatamiapo mayai 119. Kiti nyikani. Uyoga 120. Kitu changu asubuhi chatembea kwa miguu mine, saa sita kwa miguu miwili, jioni kwa miguu mitatu. Maisha ya binadamu 121. Kiwanja kizuri lakini hakifai kuweka mguu. Kipara 122. Kombe ya Sultani Ii wazi. Kisima 123. Kondoo wangu amezaa kwa paja. Mhindi 124. Kondoo wangu mnene kachafua njia nzima. Konokono 125. Kondoo za mtoto zamaliza mavuno. Jiwe la kusagia 126. Kufanya kwa ridhaa mojamoja. Kusuka mkeka 127. Kuku wangu aliangua mayai jana, lakini si kuku wala ndege. Nyoka au samaki 128. Kuku wangu amezalia miibani. Nanasi au chungwa 129. Kuku wetu hutagia mayai mikiani. Matunda 130. Kuna mlima mmoja usio pandika. Nafasi kati mdomo na pua 131. Kuna mtu mwenye tumbo kubwa aliyesimama nje. Ghala 132. Kuna ziwa kubwa ambalo limekauka na limebakiza mizizi. Chongo 133. Kunguru akilia hulilia mirambo. Mtoto akililia maziwa 134. Kwenye msitu mkubwa Napata mti mmoja tu, lakini kwenye msitu mdogo naweza kupata miwili. Watoto wa ng'ombe na mbuzi 135. Kwetu mishale na kwenu mishale. Mikia ya panya 136. Kwetu twalala tumesimama. Nguzo za nyumba L 137. La mgambo limelia wakatoka weusi tu. Chunguchungu 138. Likienda hulia, likirudi halilii. Debe aka buyu 139. Likitoka halirudi. Neno 140. Liwali amekonda lakini hana mgaga. Sindano M 141. Mama ametengeneza chakula lakini hakula. Chungu cha kupikia 142. Mbona kinakumeza lakini hakikuli? Nyumba 143. Mbona mwakunjiana ngumi bila kupigana? Mafiga 144. Mbona mwasimama na mikuki, mwapigana na nani? Katani 145. Mchana ‘ti’ usiku ‘ti’. Mlango 146. Mdogo lakini humaliza gogo. Mchwa 147. Mfalme amesimika mkuki wake hapa name nikausimika wangu kando yake, baadaye hatukuitambulisha tena. Kohozi 148. Mfalme hushuka kwa kelele. Mvua 149. Mfalme katikati lakini watumishi pembeni. Moto na mafiga 150. Mfalme wetu hupendwa sana, lakini wakati wa kumwona lazima umtoe nguo zote kwanza. Hindi 151. Mhuni wa ulimwengu. Inzi 152. Mkanda mrefu wafka mpaka pwani. Njia 153. Mke wangu mfupi, lakini huvaa nguo nyingi. Hindi 154. Mlango wa nyumba yangu uko juu. Shimo la mchwa 155. Mlima mkubwa wapandwa kuanzia juu. Sima/Ugali 156. Mlimani sipandi. Maji 157. Mlima umezuia kutazama kwa mjomba. Kisogo 158. Mlima wa kupanda kwa mikono. Mlima 159. Mlima wa kwetu hupandwa na mfalme. Nafasi kati ya mdomo na pua ya ngombe 160. Mlima wa mwenyewe hupandwa na mwenyewe. Buibui na utando wake 161. Mpini mmoja tu lakini majembe hayahesabiki. Mkungu wa ndizi 162. Msitu ambao haulii hondohondo. Mimba 163. Mti mkubwa, lakini una matawi mawili tu. Kichwa na masikio 164. Mti mnyanya mti kerekeche mti ah mti ah!. Ngoma na upatu 165. Mti wangu una matawi kumi na mawili na kila tawi lina majani kadiri ya thelathini. Mwaka 166. Mtoto asemea pangoni. Ulimi mdomoni 167. Mtu mdogo mwenye miguu mirefu ambaye aweza kutembea dunia nzima kwa dakika tano. Mawazo 168. Mvua hema na jua hema. Kobe 169. Mvua kidogo ng’ombe kaoga kichwa. Jiwe 170. Mwadhani naenda lakini siendi. Jua 171. Mwalimu analala na mwanafunzi wanamsomea. Kinyesi na inzi 172. Mwanamke mfupi hupiga kelele njiani. Kunguru 173. Mwanamke mfupi hutengeneza pombe nzuri. Nyuki 174. Mwanang’ang’a hulia mwituni. Shoka 175. Mwepesi, lakini aweza kuvunja nyumba za mji wote. Tufani 176. Mwezi wangu umepasuka. Kweme 177. Mzee Kombe akitoa machozi wote hufurahi. Mvua 178. Mzee Kombe akilia watu hufurahi. Mvua 179. Mzizi wa miti hutokea mbali. Siafu 180. Mzungu yuko ndani na ndevu ziko nje. Hindi N 181. Naitumia ngazi hiyo kwa kupandia na kushukia. Mwiba 182. Nakikimbilia lakini sikikuti. Njia 183. Nakupa lakini mbona huachi kudai. Tumbo 184. Nakwenda msituni na mdogo wangu, lakini yeye namwacha huko. 185. Nameza lakini sishibi. Mate 186. Namkimbiza lakini simkuti. Kivuli 187. Namlalia lakini halii. Kitanda 188. Namwomba atangulie lakini hukataa kabisa. Kigino 189. Nanywa supu na nyama naitupa. Muwa 190. Napigwa na mvua na nyumba ipo. Matunda ya pua/Kwapa 191. Natembea juu ya miiba lakini hainichomi. Miiba 192. Natembea juu ya miiba lakini sichomwi. Ulimi 193. Natembea na wenzangu lakini tukifika kwenye nyumba mimi hukaa mlangoni. Mbwa 194. Natengeneza mafuta lakini nimepauka sana. Mzinga was nyuki kwa nje 195. Natengeneza mbono lakini alama hazionekani. Mzinga wa nyuki 196. Ndege wengi baharini. Nyota 197. Ndugu wawili wafanana sana, lakini hawatembeleani. Macho 198. Ngoja nikumbuke. Boga changa 199. Ng’ombe wa baba watelemka mtoni. Mawe mtoni 200. Ng’ombe wa babu huchezea miambani. Mijusi 201. Ng’ombe za babu zikienda machungani hulia, zikirudi hazilii. Vbuyu 202. Ng’ombe za babu zinalala na mkia nje.Viazi vitamu udongoni 203. Ng’ombe wamechanganyika nikakosa wa kwangu. Pesa/Nyayo 204. Ng’ombe wangu ni weupe kwatoni. Katani 205. Ng’ombe wangu wote hunywa maji isipokuwa mmoja. Fimbo ya kuchunga 206. Ngozi ndani nyama juu. Firigisi 207. Nguo ivaliwayo kila siku isiyoingiwa na chawa. Nyusi 208. Nikicheka kinacheka, nikinuna kinanuna. Kioo 209. Nikienda arudi, nikirudi aenda. Kivuli majini 210. Niiita ‘baba’ huitika ‘baba’. Mwangwi 211. Nikija kwenye ndege wananifukuza, na nikienda kwenye wanyama hawanitaki. Popo 212. Nikimpiga huyu huyu alia. Utomvu wa papai 213. Nikimpiga mambusu. Puliza kidole wakati unapojikwaa 214. Nikimwita hunijibu nani. Mwangwi 215. Nikipewa chakula nala bali natema. Shoka 216. Nikitembea walio wafu huniamkia na walio hai hukaa kimya. Majani makavu na mabichi 217. Nikitembea yuko, nikikimbia yuko, nikiingia ndani hayupo. Kivuli 218. Ni kitu gani ambacho kutoa ni kuongeza? Shimo 219. Nikitupa mshale wangu mchana huenda mbali sana, lakini niutupapo usiku hauendi mbali. Jicho 220. Nikiwaambia ondokeni hukataa, lakini mjomba akitokea wote hukimbia. Umande na jua 221. Nilijenga nyumba yangu nikaiacha bila kuiezeka majani; lakini niliporudi nilikuta imekwisha ezekwa majani. Mahindi machanga 222. Nilijenga nyumba yangu yenye mlango mmoja. Jani la mgomba la nchani 223. Nilimkata alafu nikamridhia. Kupanda mbegu 224. Nilimtuma askari vitani akaniletea kondoo mweusi. Fuko 225. Nilipandia majanini nikashukia majanini. Mwiba 226. Nilipigwa na tonge la ugali la moto nilipopita msituni. Manyigu 227. Nilipitisha mkono wangu chini la ardhi, nikamshika beberu mkubwa sana. Kiazi kikuu 228. Nilipoangalia kwenye magereza ya Wazungu, nikaona wameketi juu ya mabati. Pelele 229. Nilipofika msituni nilikuta chungu cha pure kinachemka. Mzinga wa nyuki 230. Nilipoingia Rumi, alitoka mtu na wake kumi; kila mke na tundu kumi, kila tundu na kuku kumi; kila kuku na mayai kumi. Mayai, kuku, tundu, wake, kumi kumi kumi. Wangapi walikwenda Rumi? Hakuna 231. Nilipo, juu kuna miiba na chini vivyo hivyo; lakini sichomwi. Ulimi kinywani 232. Nilipokuwa mchanga nilikuwa na kijikia lakini sasa sinacho. Chura 233. Nilitembea na mwezangu naye hupita vichakani. Kivuli 234. Nimechoma fimbo yangu pakabaki pa kushikia tu. Njia 235. Nimefyeka mitende yote kiungani isipokuwa minazi miwili tu. Masikio 236. Nimejenga nyumba babu akaihamia kabla mimi sijahamia. Mjusi 237. Nimekata mti, akaja samba mwekundu akaukalia. Utomvu 238. Nimekata mti bara ukaangusha matawi pwani. Nzige 239. Nimekwenda na rafiki yangu kwa jirani, yeye akafika kabla yangu. Sauti ya nziga 240. Nimemtahiri binti wangu akatoa damu mchana kutwa. Kivuli 241. Nimempeleka kondoo wangu akatoa damu mchana kutwa. Mgomba 242. Nimemtuma mtu kumwamkua mtu, yeye amekuja, Yule aliyetumwa hajaja. Kuangua tunda Ana nazi 243. Nimemwacha mzee kikongwe mtoni anangojea mgeni kulaki. Mtego 244. Nimempandikiza mti wangu ukapeleka matawi ng’ambo ya mto. Kivuli 245. Nimesimama mbali nyikani lakini naonekani. Moto 246. Nimetembea kitambo, kukumbuka sikufunga nyumba. Dirisha Ana ufa 247. Nimetoka kutembea kutembea, nikashika ng’ombe mkia. Kata 248. Nimetupa mshale angani wala sitambui utateremsha ndege wa namna gani. Mimba 249. Nimeweka ndizi yangu, asubuhi siioni. Nyota 250. Nimezaliwa na mguu mmoja. Uyoga 251. Nimezungukwa na adui wengi, lakini siumizwi. Ulimi na meno 252. Nina kijiti change, nizidivyo kukikata ndivyo kizidivyo kuwa kirefu. Maisha 253. Nina kitu changu kitumiwacho na wengine kuliko mimi. Jina 254. Nina kitu kizuri sana nyumbani, lakini siwezi kukichukua. Dada 255. Nina kitu nipendacho ambacho hata baba, mama, dada, kaka hata na mgeni nimpendaye sana siwezi kumwazima. Mke 256. Nina mwezi ndani ya bakuli. Maziwa 257. Nina ng’ombe wangu nisipomshika mkia hali majani. Jembe 258. Nina nyumba yangu imezungukwa na mifupa. Mdomo 259. Nina pango langu lilojaa mawe. Kinywa 260. Nina watoto wangu hamsini na wote nimewavisha visibau vyeupe. Kunguru 261. Nina watoto watatu, mmoja akitoka kazi haifanyiki. Mafiga 262. Nina badilika umbo langu baada ya kila muda mfupi. Kivuli 263. Ninachimba mizizi ya mti usio na mizizi. Jiwe 264. Ninacho, nakitumia, lakini kila nikitumiapo, sikiharibu ila nakipa rangi. Maji na mkojo 265. Ninakula vitu vyote vinono lakini sikui wala sinenepi. Chungu cha kupikia 266. Ninakwenda naye na kurudi naye. Kivuli 267. Ninao mlima ambao una msitu kileleleni tu. Kichwa 268. Nitokeapo kila mmoja asema namtazama yeye tu. Jua au mwezi 269. Njia yapitwa siku zote lakini haina alama. Njia ya jua au mwezi 270. Njoo hapa nije hapo. Kiraka 271. Nne nne mpaka pwani. Matendegu 272. Nusu mfu nusu hai. Sungura alalapo 273. Nyama ndogo imewashibisha wengi wala isiishe. Kinoo 274. Nyama ya Reale haijai kikombe. Mkufu 275. Nyanya yako ana huruma kukubeba ulalapo. Kitanda 276. Nyumba yangu ina makuti tele, lakini mvua ikinyesha huvuja. Mwembe 277. Nyumba yangu ina milango mingi. Kichuguu 278. Nyumba yangu ina nguzo moja. Uyoga 279. Nyumba yangu kubwa, haina mlango. Yai 280. Nyumba yangu kubwa, haina taa. Kaburi 281. Nyumba yangu kubwa hutembelewa mgongoni. Konokono O 282. Oh! Mwanamke aliyevunja chungu mshangao wake 283. Ondoka nikae. Maji ya mfereji P 284. Paa alipenga hata pua ikapasuka. Mbarika 285. Palikuwepo watu watatu wakivuka mto. Mmoja alivuka pasipo kukanyaga maji wala kuyaona; wa pili aliyaona maji lakini alivuka bila kuyakanyaga; wa tatu aliyaona na kuyakanyaga alipovuka. Ni nani hawa? Was kwanza in Mtoto tumboni mwa mamake, was pili ni Mtoto aliyebebwa mgongoni, was tatu ni mama mwenyewe 286. Panda ngazi polepole. Sima ya ugali 287. Para hata Maka. Utelezi 288. Pete ya mfalme ina tundu katikati. Kata ya kuchukulia mizigo 289. Poopoo mbili zavuka mto. Macho 290. Po pote niendako anifuata. Kivuli R 291. Rafiki yangu ana mguu mmoja. Uyoga 292. Reli yangu hutandika ardhini. Siafu 293. Ruka Riba. Maiti S 294. Shamba langu kubwa lakini mavuno hayajazi kiganja. Nywele kichwani 295. Shamba langu miti mitano tu. Mkono wa vidole 296. Shangazi yangu ni mrefu sana lakini hafikii tumbo la kondoo. Njia 297. Sijui aendako wala atokako. Upepo 298. Sijui afanyavyo. Nyoka apandavyo mtini 299. Sina dada wala kaka, lakini baba wa huyu jamaa ni mtoto wa babangu. Ni nani huyo? Mtoto wangu 300. Subiri kidogo! Miiba 301. Sultani alipiga mbiu watu waje kufanya kazi yake lakini wakashindwa. Maji T 302. Taa ya bure. Jua au mwezi 303. Taa ya Mwarabu inapepea. Kilemba 304. Tajiri aniweka mfukoni na maskini anitupa. Makamasi 305. Tandika kitanga tule kunazi. Nyota 306. Tangu kuzaliwa kwake sijamwona asimame wala kukimbia. Mkufu 307. Tatarata mpaka ng’ambo ya mto. Utando wa baibui 308. Tatu tatu mpaka pwani. Mafiga 309. Tega nikutegue. Mwiba 310. Teke teke huzaa gumugumu, na gumugumu huzaa teke teke. Mahindi ama yai 311. Tengeneza kiwanja kikubwa kabila Fulani lije kupigania. Mbono 312. Tonge la ugali lanifikisha pwani. Jicho 313. Tukate kwa visu ambacho hakitakatika. Maji 314. Tulikaribishwa mahali na mdogo wangu, yeye akaanza kushiba kabla yangu. Kucha 315. Tuliua ng’ombe na babu, kila ajaye hukata. Kinoo 316. Tuliua ng’ombe wawili ngozi ni sawasawa. Mbingu na nchi 317. Tumvike mwanamke huyu nguo. Kuezeka nyumba 318. Tunajengajenga matiti juu. Mapapai 319. Twamsikia lakini hatumwoni. Sauti U 320. Ukimcheka atakucheka, ukimwomba atakuomba. Mwangwi 321. Ukimwita kwa nguvu hasikii, lakini ukimwita polepole husikia. Fisi 322. Ukimwona anakuona. Jua 323. Ukitaka kufahamu ana mbio, mwonyeshe moto. Kinyonga 324. Ukitembea ulimwengu wote utakosa nyayo. Mwamba 325. Ukiukata haukatiki, ukiushika haushikiki. Moshi 326. Ukiwa mbali waweza kumwona Fulani umatini. Tundu LA sindano 327. Ukoo wa liwali hauna haya. Wanyama 328. Ule usile mamoja. Kifo 329. Umempiga sungura akatoa unga. Funds LA mbuyu 330. Unatembea naye wote umjiao atakuona. Bakora 331. Upande wote umjiao atakuona. Kinyonga 332. Ushuru wa njia wKujikwaa Kujikwaa 333. Utahesabu mchana na usiku na hutamaliza kuhesabu. Nywele V 334. Viti kumi nyumbani, tisa vyakalika lakini kimoja hakikaliki. Moto W 335. Wake wa mjomba kimo kimoja. Vipande vya kweme 336. Wako karibu lakini hawasalimiani. Nyumba ama kuta zinazoelekeana 337. Wanakuja mmoja mmoja na kujiunga kuwa kitu kimoja. Matone ya mvua 338. Wanameza watu jua linapokuchwa. Nyumba 339. Wanamwua nyoka. Watu wanaotwanga 340. Wanangu wawili hugombana mchana, usiku hupatana. Mlango 341. Wanao wakati wao wa kuringa, nao ni weupe kama barafu. Nyota 342. Wanapanda mlima kwa makoti mazuri meusi na meupe. Vipepeo 343. Wanastarehe darini. Panya 344. Wanatembea lakini hawatembelewi. Macho 345. Watoto wa mtu mmoja hulala chini kila mwaka. Maboga 346. Watoto wangu wana vilemba, asio kilemba si mwanangu. Fuu 347. Watoto wangu wote nimewavika kofia nyekundu. Jogoo 348. Watoto wangu wote wamebeba vifurushi. Vitovu 349. Watu ishirini walipanda juu ya mti, wawili wakaona chungwa, watano wakalichuma, kumi wakalimenya, wote wakaridhirika mtu mmoja alile. Je, ni watu gani hao? Waliopanda ni vidole vya miguu na mikono, walioona ni macho mawili, waliochuma ni vidole vitano vya mikono, waliomenya ni vidole vya mikono yote miwili, na aliyelila ni mdomo 350. Watu waliokaa na kuvaa kofia nyekundu. Kuku, katani au mahindi 351. Watu wamehama askari wekundu wakazidi nyikani. Viroboto 352. Watu wawili hupendana sana; kati ya mchana hufuatana ingawa mmoja ni dhaifu. Usiku mdhaifu haonekani tena. Kivuli 353. Watu wote ketini tumfinye mchawi. Kula ugali 354. Wewe kipofu unaenda wapi huko juu? Mkweme Y 355. Yaenda mbali lakini haiondoki ilipo. Njia Z 356. Zilitazamana na mpaka sasa hazijakutana. Kingo za mto 357. Ziwa dogo linarusha mchanga. Chungu jikoni 358. Ziwa kubwa, lakini naogelea ukingoni tu. Moto |