FAFANUA MAANA YA FASIHI SIMULIZI KWA KUREJELEA MAONI YA WATAALAMU TOFAUTI - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Chuo (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=3) +---- Forum: Shahada (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=20) +----- Forum: Maswali na majibu (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=24) +----- Thread: FAFANUA MAANA YA FASIHI SIMULIZI KWA KUREJELEA MAONI YA WATAALAMU TOFAUTI (/showthread.php?tid=1057) |
FAFANUA MAANA YA FASIHI SIMULIZI KWA KUREJELEA MAONI YA WATAALAMU TOFAUTI - MwlMaeda - 08-28-2021
Fasihi simulizi imeelezwa kwa namna tofauti na wataalamu mbalimbali wa fasihi.
FinneganĀ (1970) anaeleza kuwa fasihi simulizi ni sanaa ambayo hutegemea msanii ambaye huiumba kwa maneno katika tukio maalumu. Katika fasili hii Finnegan hajagusia mambo muhimu katika fasihi simulizi kama vile muktadha, namna ya uwasilishaji, uhifadhi na badala yake amejikita zaidi katika ubunifu alionao msanii anayeiumba fasihi husika.
KirumbiĀ (1975:15) ameona kwamba, fasihi simulizi ni masimulizi tunayoyapokea mdomo kwa mdomo, si masimulizi yaliyoandikwa tangu awali, kwa ajili hii basi, tutaona katika fasihi simulizi kuna utumiaji wa ulumbi (ufundi wa kusema).[attachment=598] |