MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

MASWALI NA MAJIBU YA SARUFI - Printable Version
|
MASWALI NA MAJIBU YA SARUFI - Printable Version
+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Sekondari (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=4)
+---- Forum: Kidato cha tano na sita (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=44)
+----- Forum: Maswali na majibu (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=47)
+----- Thread: MASWALI NA MAJIBU YA SARUFI (/showthread.php?tid=1055)
|
MASWALI NA MAJIBU YA SARUFI - MwlMaeda - 08-28-2021
- Eleza maana ya ‘kiimbo’
Kiimbo ni sauti maalum inayojitokeza unapotamka maneno fulani. (kupanda na kushuka kwa sauti)
- Tunga sentensi mbili zinazodhihirisha uamilifu wa aina mbalimbali wa kiimbo.
Mama ameenda sokoni? -swali
Mama ameenda sokoni. -kauli
- Tunga sentensi ya hali timilifu ukitumia kiunganishi cha kibantu
Mwalimu na mwanafunzi wameenda nyumbani.
na- kiunganishi cha kibantu
wameenda – hali timilifu
- Kazi hii imekuwa ngumu kwangu. (maliza kwa ….ngumu)
Kwangu, kazi hii imekuwa ngumu.
- Andika sentensi hii kwa hali ya ukubwa, wakati uliopita
Ningepelekewa huyu ndama nyumbani ningefurahi.
Nilipelekewa hilo dama jumbani nikafurahi.
- Tunga sentensi kutumia kirejeshi cha tamati.
Kiti wakitumiacho kimevunjika.
Kirejeshi tamati ni ‘cho’
- Taja yambwa za sentensi ifuatayo :
Mjomba hakupikiwa mlo wa leo kwa bidii.
Mjomba – Yambwa tendewa:
Mlo- Yambwa tendwa
- Tunga sentensi kanushi kutumia kiambishi ‘a’
Mtoto asipolishwa vizuri, hawezi kulala.
- Andika miundo yoyote miwili ya nomino katika ngeli ya U-ZI huku ukitoa mifano
U-ny uzi-nyuzi
u-nd ulimi-ndimi
w-ny wembe-nyembe
u- ukuta -kuta
- Andika sentensi ifuatayo upya kwa kinyume
Mwafrika anapenda kutii maagizo.
Mzungu anachukia kuasi amri.
- Bainisha vitate vifuatavyo kwa kutunga sentensi moja. (alama 2)
kaza, kasa.
Mvuvi alikaza kamba alipomuona kasa akiwa ndani ya wavu.
- Taja ala za kutamkia vitamkwa vifuatavyo.
/v/g/j/t/
v- Midomo + Meno
g – Kaakaa Laini
j- kaa kaa ngumu
t- Ufizi
- Bainisha shamirisho katika sentensi: (alama 3)
Mwalimu atawasimulia wanafunzi hadithi kwa kipaza sauti
Mwalimu-shamrisho kitondo,
Hadithi- shamrisho kipozi,
kwa kipaza sauti- shamrisho ala
- Toa mifano miwili ya matumizi ya ritifaa(’)
Kuonesha king’ong’o kwa mfano ng’ombe
Kuonyesha nambari iliyoachwa kwa mfano ’99
- Walipokuwa wanasoma mgeni wa heshima alifika (andika kwa wakati ujao)
Watakapokuwa wakisoma mgeni wa heshima atafika.
- Tunga sentensi yenye ni uundo ufuatao:
S KN(N+U+N+V)+KT(T+E+E)
Mama na mtoto wake wanatembea haraka sana.
- Tunga sentensi mbili kutofautisha vitate hivi kimaana. (alama 2)
(i) Hawara
(ii) Hawala
Hawara alifukuzwa nyumbani kwa kuwa mzembe.
Alipomaliza kazi, alilipwa kwa hawala.
- Kanusha bila kutumia ‘amba’
Nitavaa nguo ambayo ni safi.
Sitafaa nguo iliyo safi.
|